SIMBA NA ASANTE KOTOKO HAPATOSHI TAIFA
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini Simba SC wanatelemka uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo kuumana na Asante Kotoko ya Ghana mchezo wa kirafiki kuadhimisha Simba Day. Asante Kotoko iliwasili jana tayari kwa mchezo huo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye mgeni wa heshima, kuelekea katika tamasha hilo kikosi cha Simba kiliwasili nchini Jumapili kikitokea Uturuki ambapo kiliweka kambi wiki mbili. Kocha mkuu wa Simba Mbelgiji Patrick J Aussems jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa atautumia mchezo huo kupata taswira ya kikosi chake, mchezo huo utaanza saa 10:00 na lengo ni kutambulisha wachezaji wapya na jezi mpya