Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2015

BIFU: PLUIJM AMKOROMEA KIBADEN, ADAI ALITAKA KUUA KIWANGO CHA KIPA WAKE ETHIOPIA

Picha
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amegeuka mbogo na kushusha lawama za wazi kwa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars, chini ya Abdallah King Kibadeni, kwa kusema kuwa anaua viwango vya wachezaji wake. Mdachi huyo akiwa na sura ya hasira, alilalamikia kitendo cha kipa wake tegemeo, Ally Mustapha ‘Barthez’ kupigwa benchi mwanzo mwisho kwenye michuano ya Kombe la Chalenji huko Ethiopia, hadi Kili inatupwa nje ya michuano hiyo kwa kile alichodai ni makosa aliyoyafanya kwenye mchezo na Algeria. Barthez alilazimika kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria, baada ya kuonekana kuwa uchochoro siku hiyo ambayo Stars ililala mabao 7-0. Akifafanua kauli yake, Pluijm alisema siku zote kocha ni sawa na mzazi, hivyo kumpotezea namna hiyo ni kummaliza kabisa kwani mwishowe atashindwa kujiamini.

BEKI AFRICAN SPORTS ATUA SIMBA, MAJWEGA NAYE KIMEELEWEKA

Picha
Dirisha dogo la usajili Ligi Kuu Bara limefikia patamu, huku Simba, Yanga na Azam FC zikionekana kuwa kivutio kipindi hiki. Wakati Yanga bado ikielekeza nguvu za usajili kumnasa mshambuliaji wa Stand United, Elius Maguli, watani wao wa jadi Simba wamemalizana na mlinzi, Novat Lufungo kutoka African Sports ya Tanga. Wakati Wekundu hao wa Msimbazi wakimalizana na  Lufungo, pia hatua za mwisho kuipata saini ya winga wa Azam FC, Mganda FC Mganda, Brian Majwega. Habari kutoka ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi, zimethibisha usajili wa Lufungo aliyelamba Sh. milioni 10 ili kuvaa jezi nyeupe na nyekundu.