BIFU: PLUIJM AMKOROMEA KIBADEN, ADAI ALITAKA KUUA KIWANGO CHA KIPA WAKE ETHIOPIA


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amegeuka mbogo na kushusha lawama za wazi kwa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars, chini ya Abdallah King Kibadeni, kwa kusema kuwa anaua viwango vya wachezaji wake.

Mdachi huyo akiwa na sura ya hasira, alilalamikia kitendo cha kipa wake tegemeo, Ally Mustapha ‘Barthez’ kupigwa benchi mwanzo mwisho kwenye michuano ya Kombe la Chalenji huko Ethiopia, hadi Kili inatupwa nje ya michuano hiyo kwa kile alichodai ni makosa aliyoyafanya kwenye mchezo na Algeria.

Barthez alilazimika kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria, baada ya kuonekana kuwa uchochoro siku hiyo ambayo Stars ililala mabao 7-0.

Akifafanua kauli yake, Pluijm alisema siku zote kocha ni sawa na mzazi, hivyo kumpotezea namna hiyo ni kummaliza kabisa kwani mwishowe atashindwa kujiamini.


“Binafsi sikupendezwa na maamuzi yake. Huku ni kumuua mchezaji, kumbuka ndiye kipa wangu tegemeo kikosi cha kwanza, yawezekana hajamtumia akiamini ndiye alikuwa tatizo katika mchezo na Algeria lakini siyo kweli….siku zote kocha ni sawa na mzazi, sasa unapomnyima chakula unatarajia nini ndani ya wiki moja zaidi ya kufa?

Ally Mustapha 'Barthez' alisota benchi mechi zote za kombe la Chalenji hadi walipotolewa kwa mikwaju ya penalti na wenyeji Ethiopia

Katika michuano ya Chalenji, Barthez amepigwa benchi katika mechi zote nne, huku kinda wa Azam, Aishi Manula akianza katika mechi tatu za makundi na Saidi Mohammed ‘Duda’ wa Mtibwa Sugar akikaa langoni katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Ethiopia ambao tulitupwa nje.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA