WENGER KUFUNGA PINGU NA MERTESACKER.

KLABU ya Arsenal inajiamini beki wake tegemeo, Per Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa muda mrefu.

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani juu ya vipengele vya Mkataba na inafahamika mazungumzo yanaendelea vizuri.

Mertesacker amedhihirisha yeye ni mwamba wa safu ya ulinzi ya The Gunners akitengeneza ukuta mgumu wa mabeki wanne akicheza sambamba na Laurent Koscielny.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza miezi 18 katika Mkataba wake wa sasa, ambao unamfanya alipwe mshahara wa Pauni 65,000 kwa wiki na kocha Arsene Wenger anataka mustakabali wake ukamilishwe haraka iwezekanavyo.


Na ikiwa mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa, Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa miaka minne, ambao utahusisha kupanda kwa maslahi yake kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Baada ya kuwa mwanzo na mgumu Uwanja wa Emirates, hatimaye beki huyo wa nguvu wa kati amefanikiwa kuteka hisia za mashabiki wa klabu hiyo ya London Kaskazini- akifanya kazi nzuri mwanzoni mwa msimu huu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA