VILLA SQUAD YAZOA MASTAA WA SIMBA, YANGA.

Uongozi wa timu ya soka ya Villa Squad inayoshiriki ligi daraja la kwanza umetuma barua kwa Bandari ya Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuomba kibali cha kumsajili kiungo Mohamed Banka anayetarajia kuichezea kwenye mzunguko wa pili.

Banka anatarajia kuichezea Villa Squad katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo unaotarajia kuanza Februari 8.

Akizungumza jana, katibu wa Villa Squad Mbarouk Kasanda alisema barua hiyo wameituma jana kwa uongozi wa timu hiyo.

"Tumetuma barua kwa ajili ya kuomba kibali cha Banka, tuna imani watatupatia," alisema Kasanda.

Alisema Villa haijaanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili kutokana na wachezaji kuwa likizo lakini jitihada za kujiimarisha, ikiwa ni pamoja na usajili zinaendelea.

Alisema kwa mujibu wa ratiba ya kocha mkuu wa timu hiyo, wachezaji wataanza mazoezi mwishoni mwa mwezi.


Aliwataja wachezaji wengine wanaotarajiwa kusajiliwa kwenye dirisha dogo kuwa ni pamoja na Nsa Job, Juma Jabu, Juma Mkongo na Godfrey Taita.

Alisema uongozi wa timu hiyo uko katika mikakati ya kuhakikisha inarejea kushiriki ligi kuu ya Bara msimu ujao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA