VIDIC ATOLEWA HOSPITALI.
Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic, ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuugua mtikiso kwenye mechi yao ya Jumapili dhidi ya Arsenal, taarifa ya klabu hicho imesema.
Vidic aliondoka uwanjani muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko baada ya kugongana na kipa wake, David de Gea.
Mlinda ngome huyo wa Serbia alipelekwa hospitalini kwa uchunguzi baada ya kupagawa kutokana na ajali hilo.
"Nemanja Vidic ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kuugua mtikiso,” taarifa hiyo ilidhibitisha.
Vidic hatarajiwi kucheza tena hadi Novemba 24 wakati United watakapo tembelea Cardiff kwenye Ligi Kuu ya Uingereza ijapokuwa hakuna muda umetengewa kurejea kwake mazoezini.
Bila ya nahodha wao, United walikamilisha ushindi wa 1-0 dhidi ya viongozi wa ligi hiyo kufunga mwanya kati yao hadi alama tano.