USHABIKI WAMPONZA SHABIKI WA ARSENAL
Shabiki sugu wa klabu ya Arsenal katika wilaya ya Iganga, Mashariki mwa Uganda anatafuta nyumba mpya baada ya kupoteza nyumba yake kwenye dau aliyowekeana na mtu mwingine kuhusu mechi kati ya klabu mbili za Uingereza, Arsenal na Manchester United.
Kabla ya miamba hao wawili kumenyana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza, Henry Dhabasani aliweka dau nyumba yake ya vyumba viwili kati yake na Rashid Yiga kwamba Arsenal wangeshinda mechi hiyo, gazeti la Observer la Uganda liliripoti.
Kwa upande wake, Yiga aliweka dau gari lake ina ya Toyota Premio pamoja na mkewe kwamba Manchester United wangeshinda.
“Wawili hao waliwekeana dau kwa maandishi, huku viongozi wa eneo hilo na mashabiki wakishuhudia mkataba huo,” gazeti hilo linasema.
Dhabasani, ambaye ana wake watatu na watoto watano, alizirai mwishoni mwa mechi hiyo baada ya Arsenal kushindwa 1-0.
Mnamo Jumatatu, mashabiki kadha wa Manchester United walifika nyumbani kwa Dhabasani na kumfurusha pamoja na familia yake.