Ruka hadi kwenye maudhui makuu

STEWART HALL WA AZAM AULA TFF.

Kauli zinazotolewa na aliyekuwa kocha wa Azam FC, Stewart Hall kuhusu kuendelea kukaa nchini licha ya kumalizana na klabu hiyo, zimeanza kuzua maswali mengi huku baadhi ya wadau wa michezo wakidai Muingereza huyo ataingia katika uongozi mpya wa Shirikisho la Soka (TFF).

Hall, kwa makubaliano na uongozi wa Azam, aliachana na Kikosi cha 'Wanalambalamba' mara tu baada ya mchezo wao wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom walioshikwa kwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wao wa Azam Complex uliopo nje kidogo mwa Jiji la Dar es Salaam.

"Naondoka Azam baada ya kupata ofa kubwa hapa Tanzania, nakuahidi kwamba nitaendelea kuwa hapa. Ninachotaka kufanya ni kitu ambacho nilikuwa nakihitaji kukifanya kwa muda mrefu, lakini sasa nimekipata," alisema Hall katika mazungumzo yake ya moja ya vyombo vya habari nchini jana.


Mmoja wa viongozi wa TFF (jina tunalihifadhi) alisema jana kuwa, huenda kocha huyo wa zamani wa timu Zanzibar Heroes na Sofapaka ya Kenya akachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo itakayoachwa na Sunday Kayuni baada ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa mwaka huu.

"Nafasi nyingi za watendaji wa kuajiriwa ndani ya TFF zitakuwa wazi kufikia Desemba 31, mwaka huu, huenda Stewart naye kajipanga kuomba moja ya nafasi hizo lakini kuwa kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars) kwa sasa ni vigumu," alisema mmoja wa viongozi wa TFF katika mahojiano maalum jana.

Kamati mpya ya utendaji ya TFF chini ya Rais Jamal Malinzi iko katika mchakato wa kusaka 'watu makini' watakaoshika nafasi mbalimbali zikiwamo za ujumbe wa kamati mbalimbali zilizovunjwa Oktoba 27 mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo.

Juzi Malinzi alisema kuwa hatakurupuka katika kuteua watu watakaoshika nyadhifa mbalimbali ndani ya uongozi wake katika shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe