SIMBA YASAWAZISHA MBILI ZA YANGA.
Klabu ya Simba imezidi kujiimarisha kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara baada ya kusajili vifaa vipya viwili, Awadh Issa, kutoka Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro na Ally Badru aliyekuwa anaichezea Canal Suez ya Misri, hivyo inakuwa kama imesawazisha baada ya watani zao kusajili wachezaji wawili pia.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema wachezaji hao kila mmoja amesaini mkataba wa miaka miwili na wanaamini uwapo wao utasaidia kukiimarisha kikosi chao ambacho kimemaliza mzunguko wa kwanza kikiwa katika nafasi ya nne.
Mtawala alisema tayari klabu yao iko katika mazungumzo na timu nyingine za Ligi Kuu ya Bara ili kuwahamishia wachezaji wengine kwa mkopo.
"Tuna nafasi moja lakini hilo si tatizo, kuna vijana wetu ambao bado wanahitaji uzoefu na kwetu Simba wamekosa nafasi ingawa ni wazuri, tutawapeleka kwa mkopo katika baadhi ya timu ambazo zimeonyesha nia ya kuwatumia," alieleza Mtawala.
Alisema Kamati ya Utendaji ya timu hiyo bado haijapanga kukutana lakini imeshaanza kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden 'King' katika ripoti yake.
Katibu huyo aliwataka mashabiki wa Simba kuwa na subira na kuamini timu yao itafanya vizuri katika mzunguko wa lala salama na kwamba tofauti ya pointi walizonazo dhidi ya watani zao si kubwa.
Badru na Issa pia ni wachezaji wa timu ya soka Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na jana mchana baada ya kumaliza kusaini mikataba ya kuichezea Simba mbele ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, walirejea visiwani humo kuendelea na maandalizi ya mashindano ya Kombe la Chalenji.