RAGE AMWEKA KANDO HANSPOPE SIMBA.


Mwenyekiti wa Simba SC Alhaj Ismail Aden Rage inaonekana kama ameamua kumweka kando mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Zackaria Hanspope katika shughuri nzima za usajili kutoka na maneno yao kupishana huku vitendo vikionekana kufanywa na Rage badala ya Hanspope.

Hivi karibuni Hanspope alisikika kwenye kituo kimoja cha redio akisema klabu yake haioni mchezaji wa kumuongeza katiia dirisha dogo hasa anayetokea hapa nchini kutokana na wote viwango vyao kufanana, pia amedai Simba haina mpango wa kusajili katika dirisha dogo.

Tofauti na kauli yake Hanspope ambaye ndiye mwenye dhamana ya kushughurikia usajili katika klabu hiyo, ambapo mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alionekana akiwasainisha wachezaji wawili Awadh Issa toka Mtibwa na Badru Ally wa Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri.


Rage alionekana katika matukio yote ya utiaji saini kwa wachezaji hao, kazi hiyo hufanywa na Hanspope ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili, kwa upande wa Yanga kazi ya utiaji saini hufanywa na Abdallah Bin Kleb ambaye hivi karibuni alimsainisha aliyekuwa kipa wa Simba Juma Kaseja na kiungo wa Ruvu Shooting Hassan Dilunga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA