PHIRI KOCHA MPYA SIMBA.
Uongozi wa Klabu ya Simba umeanza mazungumzo na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mzambia Patrick Phiri, ili kuchukua mikoba ya Abdallah Kibaden 'King', imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, zinaeleza kuwa Phiri akipatikana atasaidiana na kocha mkuu wa timu ya vijana ya Simba (Simba B), Selemani Matola.
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa, jana kwa nyakati tofauti viongozi wa Simba walianza mazungumzo na Phiri pamoja na nahodha wao wa zamani, Matola wakimtaka kuisimamia timu hiyo iliyomaliza mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya nne.
Taarifa hizo zilifafanua kuwa, kulikuwa na mipango ya kuajiri kocha kutoka Urusi lakini hali ya ukata ndani ya klabu hiyo na mafanikio aliyoyapata Matola kwa kuandaa vijana yalisitisha mikakati ya kumleta mzungu huyo.
"Wamefanya mazungumzo na Matola leo (jana) asubuhi na kesho (leo) wataendelea, ila naye tayari ameshawaambia mipango yake ikiwamo kuangalia maslahi, unajua makocha wazawa wengi wamepita hapa, lakini thamani yao haionekani licha ya kufanya kazi kubwa," alisema mmoja wa viongozi wa Simba.
Hata hivyo, Matola alisema ni mapema mno kusema lolote kuhusiana na yeye kuhamishiwa katika timu hiyo ya wakubwa.