P-SQUARE KUWASHA MOTO DAR LEO.

Mapacha Peter na Paul Okoye wanaounda kundi la wanamuziki wawili la P-Square la Nigeria wameahidi kutoa shoo kali kwa mashabiki katika onyesho la leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini, ikiwemo kutumbuiza kwa saa mbili mfululizo bila kupumzika.

Kundi la P-Squere ambalo linatikisa ulimwengu kwa singo ya 'Pesonaly', limekuja nchini kwa mwaliko wa kituo cha televisheni cha EATV na East Africa Redio; chini ya udhamini mkuu wa Vodacom na kapmuni za Hennessy na Mastermind.

Katika onyesho hilo, P-Square watasindikizwa na Lady Jaydee, Prof Jay, Jo Makini na Ben Pol ambao wote kwa pamoja jana waliahidi kutoa burudani ya kiwango cha juu katika kuchuana na wageni hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Peter alisema wamekuja nchini kutoa "shoo kali kwa mashabiki wa muziki na Watanzania wote kwa ujumla."

P-Square wanathamini muziki wa Afrika na ndio maana wanajitahidi kila siku kupiga staili ya kiafrika, alisema Peter, kwa ajili ya kuendeleza muziki kwa Bara la Afrika.

"Tunataka kuendeleza muziki wa Afrika kwa hiyo wasanii wa Tanzania tushirikiane pamoja," alisema Peter.

Alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani kabambe ya saa mbili mfululizo bila kupumnzika.

Naye Paul alisema wamefurahishwa na mapokezi ya Watanzania na ukarimu walioonyeshwa tangu wawasili "katika nchi (hii) ya kitalii" juzi usiku.

Alisema katika kulipa fadhila, P-Square itatoa burudani ambayo ni ya kwanza ya aina yake na ya funga mwaka 2013.

Aidha, aliwataka wanamuziki nchini kushirikiana pamoja ili kuhakikisha wanapeleka mbele muziki wa bara la Afrika.

"Sisi ni wamoja, tufanye kazi pamoja ili tukuze muziki wa Afrika kama ilivyo mabara mengine," alisema Paul.

Mkuu wa vipindi wa EATV Nasser Kingo alisema televisheni hiyo imejiandaa vizuri kwa onyesho hilo na kwamba usalama kwa mashabiki na ulinzi wa mali zao vitakuwepo vya kutosha.

Naye mkuu wa masoko na mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alisema wameamua kushirikiana na EATV na East Africa Radio ili kutoa nafasi kwa wanamuziki wa Tanzania kujifunza kutoka kwa Wanigeria hao.

"Hakuna asiyewafahamu P-Square walivyoitoa kimasomaso Afrika katika muziki," alisema Twisa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA