MUME WA MAREHEMU NYAWANA YAMKUTA MAKUBWA.

Kaisi Musa Kaisi (Pichani) mume wa marehemu Nyawana ambaye alikuwa akitamba kwenye muziki wa taarabu hapa nchini hatimaye yamemkuta makubwa baada ya kutoswa na kundi la wanasalamu wenzake ambao kwa sasa wana umoja wao unaofahamika kwa jina la Umoja wa Wanasalamu mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari hizi ambacho ni rafiki wa karibu na Kaisi Musa Kaisi ambaye ni mmoja kati ya wanasalamu maarufu hapa nchini kupitia vituo vya redio pamoja na magazeti alijikuta akitengwa na wenzake katika msiba wa marehemu mke wake aliyefariki kwa kuugua malaria.

Taarifa kamili zinasema kuwa Kaisi amekuwa na tabia ya kutoudhuria misiba ya wanasalamu wenzake huku ikidaiwa umaarufu ndio umemfanya ajione staa, chanzo chetu kiliendelea kusema kuwa wanasalamu wamekuwa na utaratibu mzuri wa kuudhuria misiba ya wadau wao hata kama si maarufu.

Kupitia afisa wao wa habari Salum Mfunga 'Rais wa mafukara Tz' amethibitisha habari hizo kuwa wanasalamu kwa pamoja wameamua kuachana kabisa na Kaisi na waliudhuria msiba wa Nyawana kwa sababu marehemu kabla ya kufikwa na mauti alikuwa mtangazaji katika kituo cha redio Passion.

'Ni kweli marehemu alikuwa mtangazaji Passion hivyo sisi kama wadau tuliamua kumsindikiza ndugu yetu huyo, kuhusu Kaisi kusema kweli hatuna habari naye kwani si mwenzetu tena, alianza kututenga tangia mwanzo hivyo kama umoja umeamua kuachana naye', alisema na kuongeza.


Mfunga ambaye anakubalika kwa hamasa zake amedai umoja wa wanasalamu uliikabidhi familia rambirambi yao ambapo mchango wa wanasalamu uliwezesha kupatikana kwa shilingi Laki moja na elfu Ishiriini (120,0000).

Fedha hizo alikabidhiwa mtoto mkubwa wa marehemu Nyawana na kumtosa mume wa marehemu Kaisi Musa Kaisi ambaye alionekana kuwa na huzuni, pia Kaisi Musa Kaisi inasemekana alijenga uhusiano wa kimapenzi kabla ya kufunga ndoa na marehemu Nyawana alipokuwa meneja wa kundi la taarabu la T-Moto huku ikidaiwa kuikacha ndoa yake ya awali na mkewe aliyezaa naye watoto.

Katika maisha yao mapya kati ya Kaisi na Nyawana hawajawahi kupata mtoto licha ya kila mmoja kuwa na watoto wawili nje ya ndoa yao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA