MSANII CHIPUKIZI ALIA NA MAPRODYUZA.

Msanii chipukizi wa miondoko ya kizazi kipya nchini anayefahamika kwa jina la Tozi Mchafu (Pichani) hatimaye amefunguka kulia na maprodyuza hasa kwa tabia zao za kuwabagua wanamuziki chipukizi na kuwakatisha tamaa ya kuendelea na muziki huo.

Akizungumza na Mambo Uwanjani hivi karibuni, Mchafu amedai kwamba amepata shida sana kurekodi wimbo wake mpya na umejaribu kusota kwa prodyuza zaidi ya miezi nane au tisa sasa, msanii huyo ameshangaa kuona maprodyuza kuwababaikia wasanii wenye majina wakati na wao walianza kama wao.

'Mimi nashangaa sana, maprodyuza tena hawa wanaoanza kujulikana sasa wanaonyesha ubinafai mkubwa kwetu chipukizi, inafikia hatua tunakata tamaa, utakuta unakwenda studio kurekodi unapewa taratibu zote na kulipia gharama lakini siku hadi siku unapigwa kalenda', alisema na kuongeza.

'Mimi yamenikuta katika studio moja (Jina tunalo) ambapo nimesota karibu miezi minaje au tisa, inafikia hatua msanii chipukizi unavunjika moyo, lakini uvumilivu wangu umeweza kunisaidia na sasa nimekabidhiwa nyimbo yangu lakini haijakamilika', aliendelea kulalamika.


Msanii huyo amedai vitendo vinavyofanywa na maprodyuza wa muziki wa kizazi kipya vinawakatisha tamaa (Underground) 'Unajua wasanii wenye umaarufu ambao wanababaikiwa kila sehemu walianza kama sisi, pia sisi tuko wengi kuliko mastaa hivyo maprodyuza wangeweza kutengeneza pesa nyingi kama wangetujali' alisisitiza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA