MESSI AJA NA MAAJABU MAPYA.

Lionel Messi atafanya kila awezalo kuhakikisha anapona jeraha la misuli ya paja ambalo alipata Jumapili na ambalo litamfanya akae nje ya soka kwa kati ya wiki sita na nane, mchezaji huyo wa Argentina ambaye pia ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani alisema Jumanne.

Hayo ndiyo matamshi yake ya kwanza hadharani tangu aondoke kwenye mechi mapema wakati wa ushindi wa Barca wa 4-1 katika Real Betis. Messi alisema lengo lake kuu ni kurejea mchezoni mapema iwezekanavyo na kusaidia mabingwa hao wa Uhispania katika kutafuta kikombe.

"Kama wengi wenu mjuavyo, wiki chache zijazo, nitakuwa nikifanya kila liwezekanalo nipone jeraha nililopata majuzi,” Messi alisema kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Kwangu, ni masikitiko kwamba sitaweza kuchezea timu yangu kwa sasa,” akasema mchezaji huyo wa umri wa miaka 26.

"Kwa sasa, la muhimu zaidi ni kupata nafuu vyema ili niweze kusaidia wachezaji wenzangu na kuwazawadi nyote kwa uungaji mkono ambao mmneipa kwa njia bora zaidi niwezayo, kucheza soka.”

Messi aliondolewa kwenye mechi dakika ya 19 Seville baada yake kukimbia akishindania mpira na wapinzani.


Hilo lilikuwa jeraha lake la tatu kwenye paja baada ya matatizo sawa karibu na mwisho wa msimu uliopita.

Kutokuwepo kwake si kubaya kama vile wengi wanaweza kudhani kwani kuna uwezekano kwamba atarejea kabla ya Barca kukabiliana na wapinzani wao wa kupigania taji Atletico Madrid mwezi Januari na tayari wamefuzu kwa timu 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Fowadi wa Brazil Neymar, aliyejiunga nao kutoka Santos kipindi cha kuhama wachezaji ni mchezaji mwenye uwezo wa kuwafaa sana Barca na mchezaji huyo wa umri wa miaka 21 anatarajiwa kuonyesha sababu yake kununuliwa euro 57 milioni ($76.6 milioni) wakati Messi atakuwa nje.

Raia huyo wa Argentina atakosa mechi mbili za mwisho za Barca katika dimba hilo kuu la Ulaya, dhidi ya Ajax Amsterdam na Celtic.

Pia hatacheza mechi za La Liga dhidi ya Granada, Athletic Bilbao, Villarreal na Getafe na mechi mbili za nyumbani na marudiano katika King's Cup dhidi ya Cartagena lakini anafaa kuwa amerudi tayari kwa pambano la La Liga Atletico wikendi ya Januari 11-12.

Barca wanaongoza ligi wakiwa alama tatu mbele ya Atletico na sita mbele ya wapinzani wao wa jadi Real Madrid walio wa tatu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI