MAKALA: HANSPOPE ILIBIDI AENDE NA RAGE.
Na Prince Hoza, 0772 954167
MWANZONI mwa wiki hii kamati ya utendaji ya klabu ya Simba ilitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Alhaj Ismail Aden Rage kwa madai ya kuiendesha Simba kama mali yake binafsi, pia ilitangaza kuwafuta kazi makocha wa timu hiyo Abdallah Kibadeni 'King' na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo 'Julio'.
Habari hizo zilionekana kushtua zaidi isitoshe wapenzi na mashabiki wa Simba walishuhudia usajili wa wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Zanzibar Awadh Juma na Badru Ali, Usajili huo ulifanywa na mwenyekiti wa Simba Alhaj Rage.
Hivyo kitimutimu kilichokuja kutokea kiliweza kumshangaza kila mpenda michezo nchini, licha ya mapinduzi hayo yaliyofanywa na kamati ya utendaji chino ya makamu mwenyekiti wa Simba Joseph Itang'are au mzee Kinesi yaliweza kuendana na mabadiliko mengine katika benchi la ufundi la timu hiyo.
Kikubwa kilichopelekea Simba kuingia kwenye malumbano yanayopelekea kusimamishwa kwa mwenyekiti wake ni matokeo mabaya katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Wanasimba walio wengi hawajaridhishwa na mwenendo wa timu yao kiasi kwamba waalianza kuwazomea wachezaji wao na kudiriki kufanya vurugu zilizopelekea kung'oa viti vya uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa Simba hawamtaki kocha wao Kibadeni na msaidizi wake Julio, wanasema Kibadeni na Julio ni moja kati ya sehemu inayosababisha kushindwa kufanya vizuri kwa timu yao, mashabiki hao wenye mapenzi ya kupindukia na timu yao wameonyesha waziwazi uzalendo wao ambapo wamefikia kutoa mapendekezo yao ili makocha hao watimuliwe.
Lakini mwenyekiti wa Simba Ismail Rage alionekana kuwakingia kifua makocha hao na kudai waachwe, Rage amesema kuwa Kibadeni na Julio ni makocha wazuri na wataendelea kukinoa kikosi hicho hadi mzunguko wa pili utakapomalika na wataangalia kama kuna umuhimu wa kuajiri makocha wengine.
Hilo ndio tatizo lililopo Simba, Simba hadi sasa inakamata nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 24 ikiwa imeachwa pointi nne na anayeongoza ligi Yanga, kwa wastani nafasi iliyopo Simba si mbaya sana kwani timu shiriki zipo 14 hivyo maneno ya Rage yalipaswa kuheshimika.
ETI CHANZO NI EMMANUEL OKWI
Kwa mujibu wa kaimu mwenyekiti wa Simba mzee Kinesi alitaja moja kati ya sababu zilizopelekea kumsimamisha mwenyekiti wao Rage ni kitendo chake cha kumuuza mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kwa klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia bila ya kulipwa chochocte.
Okwi alikuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Simba kuuzwa kwake kumeweza kuiathili klabu ya Simba kwani hadi sasa haijapata mbadala wake, viongozi wa Simba walioshiriki kikao cha kumng'oa Rage wamesema kwamba Rage alifanya maamuzi binafsi ya kumuuza Okwi pasipo kuhusisha kamati ya utendaji.
Mzee Kinesi aliendelea kusema kwamba walimpa muda mwenyekiti wao kufuatilia fedha zao huko Tunisia na mara ya mwisho walimtaka aende kuonana na mabosi wa timu hiyo na lazima arudi na fedha za mauzo ya Okwi, lakini danadana ziliendelea hivyo walishindwa kumuelewa mwenyekiti wao.
Lakini kama suala la Okwi ndio kigezo basi lawama zisingepaswa kuelekezwa kwa Rage peke yake, Simba iliunda kamati mbalimbali ikiwemo ya usajili inayoongozwa na Zackaria Hanspope, kamati hii ya usajili imefanya kazi nyingi zinazohusu usajili wa kikosi cha msimu huu.
Wakati Rage anauzwa Hanspope alikuwa wapi? Mara kwa mara wote kwa pamoja waliithibitishia Simba kulipwa fedha za Okwi ifikapo Septemba 30 mwaka huu, na muda ulipofika hakuna lolote lililoendelea zaidi ya kusikia Simba imewasilisha malalamiko yake FIFA.
Suala la Okwi kwa sasa limegeuka danadana, na mapinduzi yaliyofanyika dhidi ya Rage hayakuwa ya kiungwana, kama walitaka kumuondoa Rage basi Hanspope naye nje, Rage na Hanspope kwa pamoja walisimama kidete na kuwahadaa Wanasimba.
Walitangaza kikosi cha ushindi msimu huu na ukweli ulionekana katika mechi za mwanzo mwanzo kiasi kwamba Wanasimba walianza kuwa na imani na timu yao, kuteleza mechi za mwisho ndio kumeanza kutokea malalamiko huku wengine wakitaka makocha wa timu hiyo watimuliwe.
Kitaalamu kufukuza makocha kila msimu au mzunguko wa kwanza kunaweza kuiathili timu, kila kocha mpya anatumia mfumo wake hivyo wachezaji wanapata shida kuzoea mifumo tofauti katika msimu mmoja, Wanasimba wamebariki mapinduzi ya kumng'oa mwenyekiti wao kitendo ambacho kinaweza kuigawa timu.
Simba isitegemee mafanikio katika kipindi kifupi cha mwezi mmoja kwa kumleta kocha mpya, Wakati Tanzania tukililia mafanikio ya wiki moja kufuzu fainali za kombe la dunia, wenzetu walioendelea wanatumia miaka minane kutengeneza kikosi.
Uvumilivu siku zote unahitajika na Simba ilistahili kuvumilia na siyo kutimua makocha, nailaumu kamati ya utendaji kwa kile ilichokifanya hasa kumng'oa mwenyekiti wao Rage, Rage hakuwa na mapungufu yaliyopelekea kumtengenezea zengwe huku wengine wakimbeza 'Mwanasiasa'.
Sioni cha muhimu kinachomfanya Hanspope aendelee kusalia ndani ya Simba, kama Rage amefanya madudu katika mauzo ya Okwi basi Hanspope naye anahusika, ana sababu mbili au tatu kuhusika katika usajili wa Okwi na kila kitu anajua.
Siwezi kukubaliana na maamuzi ya utendaji ya Simba kwa kumsimamisha Rage, siku zote mwenyekiti ana maamuzi yake binafsi kama alivyofanya Rage, inawezekana ndani ya Simba kuna watu hawakutaka kumuunga mkono Rage katika vita vyake vya kupambana na maharamia wanaotengeneza jezi feki za klabu hiyo ambapo mheshimiwa Rage ameweza kuwabana.
Kwa sasa ukishikwa na jezi feki ya Simba unakwenda jela, wapo baadhi ya wanachama tena waliwahi kushika nyadhifa kubwa katika timu hiyo wanahusika na kufanya biashara ya jezi feki, bila shaka mtu mwenye weledi anaweza kuelewa nini kilichopelekea kusimamishwa kwa Rage.