MAKALA: CHALENJI MTIHANI WA MWISHO KWA KIM POULSEN.

Na Prince Hoza

TIMU ya taifa ya Tanzania bara maarufu Kilimanjaro Stars iliondoka jana kuelekea jijini Nairobi kushiriki fainali za mataifa Afrika mashariki na kati ambayo mwaka huu yanafanyika nchini Kenya, kikosi cha bara kiliondoka jana jioni na kuagwa kwa heshima zote.

Tumehuhudia nahodha mpya wa timu hiyo akitangazwa badala ya aliyekuwa nahodha Juma Kaseja ambaye ametemwa katikia kikosi hicho kwa sababu hakuwa na timu timu msimu huu, Kelvin Yondani beki wa kutegemewa wa mabingwa wa soka nchini Yanga ndiye aliyechukua nafasi ya Kaseja kuongoza wachezxaji wenzake ndani na nje ya uwanja.

Tuna imani kubwa kuwa timu hiyo inaweza kufanya vizuri hatimaye kurejea na kombe, Watanzania wamepoteza imani kwa timu yao hiyo hasa kutokana na matokeo mabaya iliyokuwa ikiyapata siku za hivi karibuni, kuwepo kwa wachezaji wawili wa kutumainiwa Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wanaichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kunaweza kuleta matumaini.

Lakini pia huu ni mtihani mwingine muhimu kwa kocha wa timu hiyo Mdenishi Kim Poulsen, Poulsen anahitaji mafanikio ili aweze kutuliza akili yake hasa baada ya kuandamwa mara kwa mara kutokana na kikosi chake kushindwa kuwafurahisha Watanzania.


Wachezaji wa Kili Stars ndio wanaounda kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho nacho kimeshindwa kuwafurahisha Watanzania, hivyo unakuwa mtihani wa mwisho kwa kocha huyo, tangia kuingia madarakani kwa rais mpya wa TFF Jamal Emilly Malinzi tetesi za kuajiliwa kocha mpya zilianza.

Uwezo wa Poulsen unaonekana umeshia hapo halipo na ndio maana michuano ya Chalenji inatumika kama mtihani wa mwisho, endapo timu ya Kilimanjaro itashindwa kurejea na ubingwa au kushika nafasi tatu za juu bila shaka kibarua chake kitakuwa shakani.

Tumshuhudia kufutwa kazi kwa makocha mbalimbali wanaoshindwa kuzipa mafaniko timu zao hasa zile za taifa, suala la kuinoa timu pasipo mafaniko limekuwa gumu kwa wamiliki wa timu au mashabiki, tangia kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo, morali ya mashabiki wa soka kuipenda timu yao ya taifa imeshuka maradufu.

Ingawa tatizo halijajulikana hadi sasa lakini uhamasishaji wa kocha huyo ulichangia watu mbalimbali kuishangilia timu yao ya taifa pasipo kujali Usimba au Uyanga, lakini miaka ya hivi karibuni uzalendo imepungua hasa kuiunga mkono timu yao ya taifa.

Baadhi ya mashabiki wanasema kilichopelekea kuisusa timu yao ya taifa ni mafanikio haififu tofauti na na enzi za Maximo ambapo timu ya taifa ilionekana kufanya vizuri kiasi kwamba iliweza kucheza mechi ya kirafiki na timu zenye majina makubwa duniani.

Maximo aliwaomba Watanzania kumvumilia japo miaka minane ili aweze kulikuza soka la Tanzania, kauli hiyo iliwachefua wengi ambao walikuwa na shauku ya kuiona timu yao ikicheza fainali za mataifa Afrika pamoja na kombe la dunia.

Ni sawa na mashabiki wa Simba pamoja na kamati yao ya utendaji ambao wanataka kuiona timu yao msimu huu ikitwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara, kocha wao Abdallah Kibadeni alishasema kuwa Simba haitaweza kutwaa ubingwa na alizipa nafasi Yanga na Azam kutokana na ubora wa vikosi vyao.

Lakini amshabiki wa Simba pamoja na viongozi wachache wanaojiiita wanaharakati kuamua kumsimamisha mwenyekiti wao Ismail Aden Rage ambaye amekuwa akiwakumbatia makocha hao pamoja na kuwafuta kazi kabisa Kibadeni na msaidizi wake Julio.

Leo hii Simba inamsubiri kocha mpya ili awape ubingwa, ndivyo ilivyo kwa Pulsen ambaye amechukua mikoba ya mtangulizi wake Jan Poulsen aliyetimuliwa kwa kushindwa kuipa mafanikio Stars, kushindwa kwa Poulsen mkubwa kumeibua matumaini mapya kwa Poulsen mdogo ambaye tunaye mpaka sasa.

Lakini ameshindwa kuiwezesha Stars kucheza fainali za mataifa Afrika na kombe la dunia, tunaendelea kuwa watazamaji tunaobadilishana timu za kushabiki pindi fainali za michuano mikubwa hasa kombe la dunia au Afrika inapoanza.

Sidhani kama Poulsen ataweza kufikia malengo kama yalivyo kwenye vichwa vya Watanzania, Watanzania wanataka kuiona timu yao ikicheza fainali za kombe la dunia ama mataifa Afrika, kutofika huko kunawanyima upendo na timu yao ya taifa.

Poulsen ndiye mwenye matumaini yao, Malinzi aliwaahidi Watanzania atakapofanikiwa kuingia madarakani ataifikisha Tanzania mbali, ina maana Tanzania itafanikiwa katika soka, uongozi wa Leodegar Tenga ulishindwa kuleta maendeleo ya haraka katika mchezo wa soka huku Tanzania ikiendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.

Kushindwa huko kulitokana na sera yake ya kutengeneza taasisi imara na kudumuisha utawala bora, ni kweli Tenga ameweza kuhusu hilo, kwani tumeshuhudia uundwaji wa kamati mbalimbali zilizokuwa na mamlaka ya kutatua na kusimamia kanuni zilizowekwa.

Ujio wa Malinzi unaonyesha dhamila ya kweli kuifanya Tanzania kucheza soka la ushindani, michuano ya Chalenji ni mwanzo wa hatua zake za kulelekea kwenye mafanikio, endapo Stars itaondolewa mapema ina maana Poulsen atafutwa kazi na kuletwa kocha mpya ili aweze kutimiza ndoto za Watanzania.

Ni kibarua kigumu kwa Poulsen, kwani anakwenda kushindana na timu zenye uwezo ambazo nazo zimepania kama ilivyo Stars, katika michuano hiyo Stars italazimika kucheza kwa jitihada kubwa ili kuweza kupenya na kuzifunga timu ngumu kama Uganda na Burundi ambazo mwakani zitashiriki fainali za kombe la Chan zitakazofanyika Afrika Kusini.

Tanzania ilishindwa kufuzu fainali hizo baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', matarajio yangu na Watanzania wenzangu kuiona Stars ikiwasiri nchini na kikombe cha Chalenji kama ilivyowahi kufanya hivyo mwaka 1994 ikiwa chini ya kocha mzalendo Sillysaid Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu.

Mwandishi wa makala hii ni mchambuzi katika gazeti la Mwanasoka, anapatikana kwa namba 0772 954167.  








Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA