KASEJA ATOBOA SIRI YA KUITEMA SIMBA.

Mlinda lango nambari moja nchini Juma Kaseja ametoboa siri ya kuikacha klabu yake ya zamani Simba na kumwaga wino kwa vijana wa Jangwani maarufu Yanga kwamba amefuata maslahi mazuri ambayo ilikuwa ngumu kupata angekuwa Simba.

Akizungumza na Mtandao huu, Kaseja amesema kuwa Yanga ndio timu kubwa hapa nchini na inayolipa vizuri tofauti na klabu nyingine zilizomuhitaji msimu huu, anasema katika kipindi chake alichokaa bila kuwa na timu msimu huu timu nyingi zilimfuata lakini hakuna iliyofikia dau la Yanga.

Aidha kipa huyo amewaondoa hofu mashabiki wa Simba na kuwaambia mpira kazi yake na asingeweza kuikacha ofa ya Yanga, amedai yeye ni mchezaji na mpira kazi yake hivyo hawezi kukaa ofa yoyote yenye maslahi mazuri kama aliyopewa na Yanga.

Cha zaidi Kaseja amewataka mashabiki wa Yanga kumpa muda ili aweze kujifua na timu hiyo kabla hajashuka dimbani kuanza kuichezea kwa mara nyingine, Kaseja aliwahi kuichezea Yanga mwaka 2009 kwa msimu mmoja kisha kurejea katika klabu yake ya zamani ya Simba.


Kwa sasa Kaseja amesaini Yanga na ataanza kuichezea katika mzunguko wa pili mwakani pamoja na michuano ya kimataifa, Yanga itashiriki ligi ya mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa bara msimu uliopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA