JANJA YA RAGE YABAINIKA, YADAIWA ANATUMIA MASHABIKI WA YANGA KUMLAKI.
Imefahamika kwamba mwenyekiti wa Simba ambaye hivi karibuni alisimamishwa na kamati ya utendaji Ismail Aden Rage, inasemekana amekuwa akitumia ujanja wakati wa mapokezi yake na kulakiwa na watu wengi wanaokwenda na vuvuela huku wakimbeba juu juu.
Sasa imebainika kuwa mwenyekiti huyo wa Simba anatgumia kundi la mamluki ambao wengineo ni mashabiki wa kutupwa wa Yanga ambao hudiriki kuvaa jezi za Simba na kumuunga mkono, aidha ujanja huo umebainika na Simba wameandaa mpango rasmi wa kumng'oa Msimbazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjumbe mmoja wa kamati maalum ndani ta tawi moja maarufu jijini Dar es Salaam lkenye ushawishi mkubwa ndani ya klabu hiyo anasema kuwa ujanja wa Rage umejulikana hivi karibuni baada ya wapambe wake kuwakusanya mashabiki wa soka ambao wengine ni Yanga.
'Ni kweli Rage ametumia mashabiki wa soka na kujifanya wanampenda sana kisha kwenda uwanja wa ndege kumpokea, sisi wengine tunakaa nao na wengine ni marafiki zetu ambao tunawafahamu kama Yanga damu na wametuambia kuwa walialikwa na Rage ili kuwaonyesha Simba', alisema mumbe huyo.
Aidha amedai ili Simba imuondoe katika wadhifa huo ni lazima wajumbe wa kamati ya utendaji wachukue hatua nzito na kukubali kujitoa mhanga, amesema njia pekee ya kumuondoa Rage ni wajumbe wa kamati ya utendaji wote kwa pamoja wajizuru nyadhifa zao ili Rage ashindwe kuwa mwenyekiti kamili.