JAHAZI LA MAN UNITED LAZIDI KUZAMA.

MCHEZAJI Kim Bo-kyung aliyetokea benchi alifunga bao dakika ya mwisho na kuinusuru Cardiff kuzama nyumbani kwa kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester United.

Wayne Rooney, ambaye alistahili kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mapema kwenye mchezo huo, aliifungia United bao la kuongoza dakika ya 15 kabla ya Fraizer Campbell kusawazisha dakika ya 33.

Kona maridadi ya Rooney iliunganishiwa nyavuni na Patrice Evra dakika ya 45 na United ikaonekana kama itashinda, lakini Kim akaja kuharibu mambo mwanzoni mwa dakika nne za nyongeza akimalizia mpira wa adhabu wa Peter Whittingham.


Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra, Fellaini, Cleverley, Valencia, Rooney, Januzaj/Welbeck dk68 na Hernandez/Giggs dk73.

Cardiff: Marshall, Theophile-Catherine, Caulker, Turner, Taylor, Cowie, Medel, Mutch/Kim dk77, Whittingham, Odemwingie/Noone dk65 na Campbell/Cornelius dk84.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA