IVO MAPUNDA ATEMWA GOR MAHIA

Tetesi za kutua kwa kipa wa zamani wa Moro United, Prisons na Yanga Ivo Mapunda ambaye anaichezea Gor Mahia ya Kenya katika klabu ya Simba huenda zikatimia baada ya kipa huyo kutokuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Kenya.

Ivo Mapunda anatajwa kuwemo katika kikosi cha Simba kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara, taarifa zilizothibitishwa na chanzo chetu cha habari zinasema kuwa kipa huyo mzoefu aliyeitwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Zimbabwe kesho hatoongezewa mkataba mwingine na Gor Mahia.

Kwa sasa Ivo anasugua benchi kama kipa namba mbili hivyo uongozi wa Gor Mahia umeamua kutomuongezea mkataba mwingine mchezaji huyo badala ya huu wa mwanzokumalizika rasmi, Ivo ameiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kenya lakini amejikuta katika wakati mgumu hasa anapoanzia benchi.

Kulingana na taarifa hiyo inaweka wazi nafasi yake kubwa kutua kwenye ligi kuu ya bara na Simba inatajwa kama timu pekee inayoweza kumsajili, lakini mtandao huu ulipoamua kumtafuta kipa huyo na kuzungumzia mikakati yake kama ataendelea kukipiga na Gor Mahia kwa mara nyingine.

Ivo amesema yeye kama mchezaji na kazi yake ni mpira hivyo timu yoyote ile ikiwa tayari kumsajili atakuwa radhi kwenda, anadai mkataba wakena Gor umemalizika hivyo milango iko wazi kwa timu yoyote inayomtaka imsajili.


Amedai yeye bado hajafanya mazungumzo yoyote na Simba wala timu nyingine ila meonyesha kuwa yuo tayari kuzungumza nao kwa vile mkataba wake na waajili wake umemalizika, hata hivyo Simba imeonyesha nia ya kumsajili kipa huyo kufuatia ripoti ya benchi la ufundi kuhitaji kipa, beki yakati, kiungo na mshambuliaji.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA