GERRARD AMPUUZA FERGUSON.

Nahodha wa Uingereza Steven Gerrard amepuuzilia mbali madai ya meneja wa zamani wa Manchester United Alex Ferguson kwamba kiungo huyo wa kati wa Liverpool si “mchezaji nyota.”

Ferguson alitoa madai hayo kwenye tawasifu yake, ambayo ilichapishwa mwezi uliopita, lakini Gerrard anasema majaribio ya raia huyo wa Scotland ya kutaka kumnunua ni thibitisho tosha kwamba alithamini sana uwezo wake.

“Sikizeni, ana haki ya kuwa na maoni yake,” Gerrard aliambia jarida la Jumanne la gazeti la Uingereza la Daily Mail.

"Mimi ni shabiki wake; yeye ni mmoja wa mameneja bora zaidi duniani. Sipotezi usingizi kutokana na hilo. Katika maisha yangu ya soka, nimepokea pongezi kutoka kwa watu wa kila aina – yeye akiwa mmoja wao – na huwa nazipokea.

“Nimepokea pongezi za kushangaza kutoka kwake na alijaribu kuninununua, wakati mmoja. Labda hata mara mbili.

“Kwangu, la muhimu zaidi ni lile (meneja wa Liverpool) Brendan Rodgers na (meneja wa Uingereza) Roy Hodgson wanafikiria. Ninafikiri wamefurahishwa sana name na hilo tu ndilo laweza kunitia wasiwasi.


Gerrard, 33, anatarajiwa kuchezea Uingereza mechi yake ya 108 katika emchi za kirafiki dhidi ya Chile na Ujerumani, hatua itakayomfikisha kiwango sawa na nahodha aliyeshinda Kombe la Dunia 1966 Bobby Moore.

"Kuchezea taifa mechi 107 si jambo mbaya kwa mtu ambaye si nyota, si ndivyo?” akaongeza.

“Sikutarajia kucheza mechi nyingi kiasi hiki. Nilipocheza mechi yangu ya kwanza, nilijiwekea lengo la mechi 50 na kufunga mabao 10 kama ningeweza. Kwa hivyo kupata mechi 107 ni jambo ambalo najivunia sana, hasa kuungana na wachezaji wasifika.”

Rodgers alidai wiki iliyopita kwamba Gerrard huenda astaafu baada ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka ujao, lakini mchezaji huyo alisema kwa sasa hataki kufikiria kuhusu yajayo.

“Kwangu lengo langu ni: naweza kusaidia timu yangu ifike robofainali?” alisema.

“Sijafikiria sana kuhusu nini nitafanya baada ya Kombe la Dunia. Nafikiria tu kwenda na kujivunia Kombe la Dunia. Litakuwa jambo la kusisimua kuwa Brazil.

"Nina furaha sana kuwa nilisaidia timu yangu kufika huko, ni ufanisi mkubwa. Kwa sasa, mtazamo wetu unafaa kubadilika na kuwa: tunaweza kufanya nini tukifika huko?”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA