CAMEROON YAIDUWAZA TUNISIA.

TIMU ya taifa ya Cameroon imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuifumua kwa mabao 4-1 Tunisia jioni ya leo kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, Cameroon.

Mabao ya Pierre Webo dakika ya nne, Benjamin Moukandjo dakika ya 30 na mawili ya Jean Makoun dakika za 66 na 86 yametosha kuwahakikishia Simba Wasiofungika kucheza fainali hizo kwa mara ya saba.

Bao pekee la Tunisia lilifungwa na Ahmed Akaichi dakika ya 50. Kocha wa Cameroon, Volker Finke alifanya mabadiliko matatu katika kikosi chake kutoka kile kilichotoa sare ya bila kufungana na Tunisia katika mchezo wa kwanza.

Bennoit Assou-Ekotto, Stephane Mbia na Benjamin Moukandjo walianza kwenye kikosi cha kwanza badala ya Nyom, Nounkeu na Joel Matip. Samuel Eto’o alianza katika safu ya ushambuiaji pamoja na mkongwe Pierre Webo.

Ruud Krol, naye kwa upande wake alibadilisha wachezaji wawili baada ya kushindwa kupata bao mjini Rades mwezi uliopita. Karim Haggui na Fakhreddine Ben Youssef walichukua nafasi za Sami Allagui na Alaeddine Yahia.


Cameroon sasa inaungana na Nigeria na Ivory Coast kujihakikishia nafasi ya kwenda Brazil mwakani.

Kikosi cha Cameroon kilikuwa: Itandje; Nkoulou, Chedjou, Mbia/Nounkeu dk70, Assou-Ekotto, Song, Makoun, Enoh, Moukandjo/Nguemo dk83, Webo/Choupo-Moting dk63 na Eto’o.

Tunisia: Chrifia; Derbali, Mikari, Haggui, Benyoussef, Ragued, Yahya/Allagui dk74, Chikhaoui/Camus dk46, Ben Youssef, Chermiti/Akaichi dk46 na Khalifa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA