ABEL DHAIRA ATEMWA RASMI SIMBA.

SIMBA SC inatafuta kipa mzuri wa kumsajili katika dirisha dogo, wakati huo huo inafikiria kuachana na kipa wake, Mganda, Abbel Dhaira ikibidi mapema iwezekanavyo au mwishoni mwa msimu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema leo kwamba, kutokana na kanuni mpya ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu ujao ya wachezaji watatu kutoka watano, hawatahitaji kipa mgeni.

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba kwa sababu hiyo lazima waachane na Dhaira mwishoni mwa msimu, au kama atapata timu hata sasa ambayo itakuwa tayari kuilipa Simba, watamuuza.

Poppe amesema kwa sasa Simba SC tayari inasaka kipa atakayekwenda kuwa pamoja na makipa wa wazawa, Abuu Hasimu na Andrew Ntalla.

“Niseme wazi, tunatafuta kipa. Huu ni mchakato makini sana na hatutaki kurudia kosa. Tunatafuta kipa mzawa, kwanza awe mwaminifu na mwenye uwezo mkubwa,”alisema.

Kuhusu habari kwamba, klabu hiyo inabadilisha benchi la Ufundi, Poppe amesema kwamba huo si ukweli kwa sababu hakuna kikao chochote kilichoketi kujadili suala hilo.


“Ripoti ya kocha (ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu) ndiyo kwanza inafika leo, wala hakuna kikao kilichoketi kuijadili, sasa hizo taarifa zinatoka wapi?”alihoji Poppe na kuongeza; “Sisi tunajua kuna hizo presha za kufukuza makocha, lakini hatujui haswa zinatoka wapi, mimi ninaomba nyinyi Waandishi muache kuvuruga wakati huu,”alisema.

Wakatu huo huo: Viongozi wa matawi yote Dar es Salaam wanatarajiwa wanatarajiwa kukutana makao makuu ya klabu Ijumaa asubuhi, kujadili marekebisho ya Katiba, mchakato unaoendelea vizuri hivi sasa klabu hiyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA