Na Salum Fikiri Jr DAR ES SALAAM KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC imefanikiwa kumsainisha winga machachari wa Medeama ya Ghana Enock Atta Agyoi kwa mkataba wa miaka miwili. Atta alikuwa tishio kwa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC katika mchezo wa makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama, katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1. Ina maana Ataa ataitumikia Azam FC msimu ujao na katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Azam itakutana na Yanga katika uwanja wa Taifa
Kwa habari na matangazo tunapatikana Kariakoo jijini Dar es Salaam au piga +255 652 626627 au +255 755 522 216 barua pepe princehoza@gmail.com