Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa mwisho wa kundi A kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na Medeama ya Ghana utakaofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam hatimaye watu hawataingia bure kwani kiingilio kimetajwa.
Viingilio vimetwajwa ambapo VIP A watalipa Tsh 30, 000 na VIP B watalipa Tsh 20, 000, jukwaa la Orange watalipa Tsh 10, 000 na mzunguko Tsh 5000.
Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili ifufue matumaini ya kusonga mbele, mabingwa hao wa bara wameshapoteza mechi zao mbili dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya DRC.
Kikosi hicho cha Wanajangwani kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Boko veterani