Na Mwandishi Wetu, DODOMA
Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kipya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipindi cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho.
Wasanii hao wameyasema hayo mjini Dodoma walipofanya tamasha la Usiku wa Wasanii kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi uwenyekiti wa chama hicho na kumuachia uongozi Rais John Magufuli.
PICHA ZOTE NA EDWIN MJWAHUZI