Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Simba umeonyesha nia ya kumkabidhi klabu hiyo mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji "Mo".
Mambo Uwanjani imezipata taarifa za ndani kabisa ambazo zinasema kwamba Mo anakabidhiwa timu hiyo Julai 30 mwaka huu ambapo kutafanyika mkutano mkuu wa wanachama.
Katika mkutano huo, wanachama wa Simba wataamua wenyewe kama klabu yao iendeshwe kisasa yaani kampuni ama iendelee na mtindo uleule wa wanachama.
Endapo Simba itachagua kuwa kampuni basi ni sawa kama wamempa klabu hiyo Mo ambaye ameonyesha nia kubwa ya kuinunua timu hiyo, Mo anataka kuinunua Simba kwa shilingi Bilioni 20 ni sawa na kuinunua Simba kwa asilimia 51 na hisa nyingine atawaachia Simba wenyewe