Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO mkabaji na fundi Jonas Gerald Mkude ametimka tena katika kikosi cha Simba na kuelekea nchini Afrika Kusini kujaribu bahati yake nyingine ya kucheza soka la kulipwa.
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinasema kiungo huyo ameondoka Simba wiki iliyopita kuelekea Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu moja inayoshiriki Ligi kuu nchini humo.
Hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo mkabaji kwenda kufanya majaribio nchini Afrika Kusini, Awali alijiunga na Bidvest Wits lakini alishindwa, na sasa ameenda tena kujaribu bahati yake.
Mchezaji huyo hakuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 29 wa Simba walioingia kambini mjini Morogoro, Simba imeweka kambi Morogoro ikiwa tayari kabisa kujiandaa na msimu ujao wa Ligi kuu bara