Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
TIMU ya JKT Ruvu imeamua kuachana na kocha wake mkuu Abdallah King Kibaden Mputa na kumpa mikoba hiyo mchezaji wa zamani wa Mlandege Malale Hamsini.
Kibaden aliyekuwa akiinoa timu hiyo na kuikoa isishuke daraja, atakuwa mkurugenzi wa ufundi na atakuwa akidili zaidi na timu za vijana, kwa mujibu wa mtoa taarifa hizi anasema kuwa Malale Hamsini ataweza kukinoa kikosi hicho na kufanya vizuri msimu ujao.
Kibaden pia amewahi kuzinoa Simba, Manyema, Ashanti, Kagera Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars