MAONI: TFF WAMESAHAU MAJUKUMU YAO

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

KAZI kubwa inayotakiwa kufanywa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuendeleza soka hapa nchini, pia kazi yao nyingine ni kuhakikisha maadili yanakuwepo kwenye mchezo huo.

Maadili yenyewe ni usimamizi bora, na haki kwa mashindano yote wanayosimamia, kwa bahati mbaya TFF ya sasa inaongozwa na rais wake Jamal Malinzi imeshibdwa kusimamia vyote hivyo.

Malinzi ameshindwa kufuata nyayo za mtangulizi wake Leodegar Chila Tenga ambaye ameondoka TFF lakini bado anakumbukwa kutokana na mema yake aliyoyafanya.

Malinzi ameshindwa kusimamia maadili ambapo inafikia watu wa ngazi ya chini wanashindwa kuwaheshimu viongozi wao, kwa mfano soka la Tanzania mwaka huu limegubikwa na kashfa ya rushwa ambapo Shirikisho hilo nalo limetajwa kuhusika.

Likiwa tayari limeshawapa baadhi ya watu adhabu kubwa ikiwemo kuwafungia maisha makocha na viongozi wa timu, pia wapo baadhi ya wachezaji nao wameadhibiwa.

Hii yote imetokana na uuzo uliopo ndani ya Shirikisho hilo la kandanda hapa nchini, wakati TFF ikishindwa kusimamia vema masuala yake, imejikuta ikilumbana na wasemajj wa vilabu.

Hivi karibuni msemaji wa klabu ya Yanga alilijia juu Shirikisho hilo na hasa kutokana na kitendo chao cha kukaa na zawadi yao kama mabingwa wa kombe la FA, Yanga walipaswa kukabidhiwa kitita chao cha shilingi Milioni 50.

Lakini hadi sasa bado hawajalipwa, kitendo hicho kimemfanya msemaji wa Yanga Jerry Muro kulalamika, TFF wamemtia hatiani Muro wakidai anawachafua wakati ni ukweli .mtupu aliosema.

Pia Muro amenanga tena TFF kwa kitendo chao cha kukalia vifaa vyao vya michezo walivyokabidhiwa na Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, Yanga ilipaswa kupewa vifaa hivyo kabla hata haijacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.

Lakini Shirikisho hilo likakalia vifaa hivyo mpaka ilipowakabidhi kwa mbinde tena ikijiandaa kucheza na TP Mazembe Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kwakweli TFF hii ya Malinzi imechoka wacha tuseme ukweli.

Malinzi na watu wake pale TFF wameshindwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu mashindano yoyote yale, kila tunapofikia kushiriki kombe la Dunia, Mataifa Afrika na kombe la Chan Tanzania tumekuwa wasindikizaji.

Kwa kifupi hatuna timu ya taifayenye spidi kama ile ya mtangulizi wake Tenga ambayo kidogo ilifanikiwa kututoa kimasomaso kwa kufuzu fainali za Chan mwaka 2008, Malinzi ameona ni bora kuiingiza TFF kwenye migogoro na vilabu.

Leo hii amemfungia Muro kwa kosa la kuwaambia ukweli kesho atakuja kuifungia Yanga au Simba kama itadai zawadi yake ya ubingwa wa bara kwani tayari wameonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa kuwapa Yanga zawadi yao ya  ubingwa wa kombe la FA