SAMATTA ALIZWA DAR

Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM

BABA mzazi wa mshambuliajj wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, mzee Ali Samatta amesikitikia kitendo cha baadhi ya watu kutumia jina la mwanaye Mbwana Samatta na kujinufaisha pasipo ridhaa yake mwenyewe.

Akizungumzia hilo hivi karibuni, mzee Samatta ambaye mwanaye Mbwana anakipiga Genk ya Ubelgiji, amelalamika kuwa kuna baadhi ya watu wameandika jina la mtoto wake kwenye miradi yao ya biashara wakati kufanya hivyo ni kosa.

"Ilipaswa wamshirikishe Samatta au familia yake, kuna baadhi ya mabasi yameandikwa Samatta pamoja na kubandika picha yake kubwa, pia yapo naadhi ya maduka yanatumia jina la Samatta, tutaanzisha msako mkali na tutakayemkuta anaendelea kutumia jina la mwanangu tutamkuchukulia hatua za kisheria", alisema