YANGA WAAPA KUIANGAMIZA MEDEAMA

Na Shafih Shafih, DAR ES SALAAM

KLABU bingwa ya soka Tanzania bara Dar Young Africans imewaahidi Watanzania iwe isiwe lazima wachomoze na ushindi itakapocheza na Medeama ya Ghana mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga na Medeama watacheza Jumamosi katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kiingilio cha kuiona mechi hiyo ni shilingi 3000, Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili waweze kufufua matumaini yao ya kutinga Nusu fainali.

Tayari mabingwa hao wa bara, wamepoteza mechi mbili za mwanzo katika kundi A ikianza kucheza ugenini huko Algeria, Yanga ilifungwa 1-0 na Mo Bejaia  pia ikafungwa tena 1-0 nyumbani na TP Mazembe, endapo itapata ushindi itafufua matumaini