Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Yanga SC umetangaza kumzuia kocha wake Mholanzi Hans Van der Pluijm kwamba hawezi kuondoka ndani ya klabu hiyo hata kama kuna timu imemuahidi donge nono.
Yanga wamefikia maamuzi hayo kufuatia taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao kwamba kocha huyo anatakiwa na timu moja ya barani ulaya.
Pluijm ambaye ni mshindi wa tuzo ya kocha bora wa Tanzania, ameonekana kuzichachafya timu mbalimbali nchini na kufikia hatua ya kuionea gere Yanga ambayo imetwaa mataji yote makubwa nchini mwaka huu ikiwa chini yake.
Tayari uongozi wa Yanga umefanikiwa kimbakisha kocha huyo kwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili utakaomfanya asalie katika kikosi hicho hadi mwaka 2018