Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
WAPINZANI wa Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Medeama ya Ghana inatarajia kuwasili nchini kesho Alhamisi ambapo Jumamosi ijayo watakutana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Timu hizo zinakutana katika raundi ya tatu na ya mwisho katika mzunguko wa kwanza huku zote zikipepesuka, Yanga wenyewe wanashikilia mkia wa kundi A wakiwa hawana pointi hata moja.
Medeama nao wana pointi moja, hivyo mchezo wa Jumamosi unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua kwa sababu kila timu inahitaji matokeo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea hatua ya Nusu fainali