SIMBA YAIBOMOA TENA AZAM

Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM

BAADA ya kufanikiwa kumsana mshambuliaji hatari Ally Ame 'Zungu', Klabu ya Simba imeendelea kuibomoa Azam, Na safari hii ikifanikiwa kumnasa mlinda mlango mahiri Mwadini Ally Mwadini ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Habari zenye uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, Mwadini amesainishwa mkataba wa miaka miwili na atakipiga kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2018.

Mwadini hakuwa na wakati mzuri alipokuwa Azam ambapo alikuwa akiwekwa benchi la kipa bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 Aishi Manula, hata hivyo Mwadini asingeweza kurejea langoni kwani timu hiyo imemleta kipa wa kombe la Dunia raia wa Ivory Coast