JERRY MURO ALA KITANZI MWAKA MMOJA NA TFF

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la kandanda nchini TFF leo limemtia hatiani Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa muda wa mwaka mmoja.

Taarifa zilizopatikana kutoka TFF zinasema Muro atatumikia adhabu hiyo kuanzia leo na kesho TFF itaweka bayana kila kitu.

Afisa wa Habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas amesema kesho watatangaza kilichotokea kwenye kikao cha leo kilichoamua masuala mbalimbali yanayowahusu wanamichezo, Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Muro ameadhibiwa mwaka mmoja baada ya kusikika akiitunishia misuli TFF