Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
KIPA raia wa Ivory Coast aliyepata kutamba na klabu ya Asec Mimosas, Daniel Yeboah Tetch amewasili nchini leo na atasaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo kisha kuondoka zake.
Hii ina maana atamrithi kipa wa timu hiyo Aishi Manula ambaye kwa kipindi chote alikuwa langoni peke yake pasipo kupata upinzani wowote wa namba.
Yeboah kipa aliyepata kucheza kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast iliyoshiriki fainali za kombe la dunia