Na Mwandishi Wetu, TANGA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Christopher Mhenga A K A Mkola Man amesema kuwa yeye si muumin wa freemason kama watu wanavyodhani na amewataka wale wote wanaomdhania wasifanye hivyo.
Mkola Man anayetamba na wimbo wake mpya uitwao 'Kitabu cha historia', amedai kuna watu wanamuogopa wakidhani freemaso , pia anakosa ushirikiano kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na imani hiyo iliyoota mizizi kwake.
Msanii huyo mwenye maskani yake Hale mkoani Tanga, ameongeza kuwa kuna watu wanampigia simu kutaka waunganishwe kwenye imani hiyo lakini yeye hausiani kabisa na mtandao huo na wala hajui walipo, "Mimi sio freemason na wala siwajui walipo nashangaa kuhusishwa na freemason", alisema.
Aidha msanii huyo amedai yupo mbioni kutengeneza video ya wimbo wake mpya wa Malavidavi Time aliourekodi jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka huu