STAA WETU: MATTEO ANTONY SIMON, MKOMBOZI WA YANGA ALIYEIBEBA KIMATAIFA

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

WENGI wanajua mashujaa wa Yanga ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko, Lakini wanashindwa kufahamu kwamba Yanga SC inaye shujaa ambaye si mwingine ni Matteo Antony Simon.

Huyo ni mshambuliaji wa Yanga ambaye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea KMKM ya Zanzibar, Matteo ilikuwa asajiliwe na Simba lakini kama unavyofahamu vigogo hao wa soka nchini wamekuwa na kawaida ya kunyang' anyana wachezaji.

Hatimaye Matteo akatua Yanga ingawa hakuwashangaza mashabiki wa timu kwakuwa hakuwa maarufu, mshambuliaji huyo aliyeonekana msumbufu tangia akiwa na kikosi cha KMKM, hakuwa katika kikosi cha kwanza cha Yanga kinachonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm.

Matteo alikuwa akianzia benchi na hii yote inatokana na Yanga kuwa washambuliaji wengi ambao wamekuwa msaada mkubwa kwenye klabu hiyo ambayo msimu uliopita iliweza kukusanya vikombe vyote vikubwa hapa nchini.

Yanga imeweza kuchukua Ngao ya Hisani ikiwafunga Azam FC kwa mikwaju ya penalti 8-7, pia imetwaa ubingwa wa ligi kuu bara pamoja na kombe la FA, Yanga imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kabla haijaingia hatua hiyo, Yanga ilianza kucheza michuano hiyo kuanzia raundi ya awali, Yanga ilianzia michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo iliwatoa Cerce de Joachim ya Mauritius.

Baadaye ikaifungasha virago APR ya Rwanda, kisha Yanga ikaondoshwa na Al Ahly ya Misri ambapo ikaangukia kombe la Shirikisho barani Afrika, hapo ndipo ilipojikuta inakutana na Sagrada Esparanca ya Angola.

Mchezo wa kwanza ulipigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, alikuwa Simon Msuva ndiye aliyepeleka furaha Jangwani kwa bao lake tamu la kuongoza.

Yanga ilipata bao hilo kunako kipindi cha pili na siku hiyo ilionekana kukosa mabo na hasa kukosekana kwa mshambuliaji wake tegemeo Mzimbabwe Donald Ngoma, kipindi cha pili Yanga walianza kusherehekea mabao, Matteo Antony Simon alipiga shuti kali la umbali wa mita 40 ambalo lilikwenda moja kwa moja wavuni.

Kwa maana hiyo Yanga iliwatoa Sagrada kwa jumla ya mabao 2-1 kwani katika mchezo wa marudiano uliofanyika Angola Yanga ililala 1-0 lakini goli la Matteo halikuweza kusawazishwa hivyo nyota huyo Mzanzibar anakuwa shujaa wa Yanga na ndiye aliyeivusha Yanga kimataifa



Matteo Simon Antony mwenye rasta akishangilia bao lake muhimu lililoivusha Yanga