Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
SIMBA SC sasa ni kama inamrudisha kocha wake wa zamani Mcroatia Zdravko Logarusic hasa baada ya kuipa mwaliko timu yake mpya ya Interclube ya Angola ambapo sasa itakuja kucheza na Simba katika tamasha la Simba Day katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Awali Simba iliialika Gor Mahia ya Kenya lakini sasa imeamua kuialika Interclube ya Angola moja kati ya vilabu vikubwa nchini humo, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema leo kwamba Simba itacheza na Interclube na itatambulisha kikosi chake chote.
Aveva amedai mbali na kutambulisha kikosi kipya, Simba pia itatambulisha jezi zake mpya itakazotumia kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba itafungua na Ndanda FC 'Wana-Kuchele'