Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Quality Group inayomilikiwa na bilionea Yusuph Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC imetangaza kuinunulia ndege pamoja na basi kubwa la kisasa klabu hiyo.
Quality Group itafanya hivyo hivi karibuni hasa baada ya kuingia mkataba wa kuifadhili Yanga kufuatia kuvunjika kwa mkataba wao na TBL, Manji amesema Yanga itanunuliwa ndege yake binafsi ambayo itawasaidia kwa safari zao za hapa na pale.
Hii itakuwa kwa mara ya kwanza kwa klabu ya soka hapa nchini kumiliki ndege yake binafsi, na endapo Yanga itanunua ndege italingana na TP Mazembe ya DRC inayomilikiwa na bilionea Moise Katumbi