MICHANO; MR CHEKA ALISAHAU KAMA KUCHEKA NA KULIA YOTE NI MAKELELE

Na Mkola Man, TANGA

YAP....yap...yap.Michano ya leo inamchana msanii wa muziki wa bongofleva mkazi wa Dar es Salaam lakini mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro anajulikana kwa jina la Anselin Malembo zamani alikuwa akijiita Ans B.

Huyu jamaa alitoka na wimbo mmoja aliomshirikisha msanii wa TMK Wanaume Family Mheshimiwa Temba, wimbo huo uliitwa Mr cheka ambao ukatamba vilivyo.

Jamaa baada ya kuona ametusua akaanza kujisahau na kucheka, akawa kama fisi aliyeona mzoga uliouawa na Simba badala ya kula na kuondoka zake kisha kujipanga na kutafuta wa kwake akaanza kucheka  kumbe kucheka na kulia yote ni makelele.

Mr Cheka alijua muziki ule alioutoa umetamba kwa sababu yake  kumbe Mheshimiwa Temba ndio kaubeba ule wimbo na ndio maana akauweka katika albamu yake  Mr Cheka hivi karibuni katoa wimbo mpya unaitwa Nacheka.

Kwa maono yangu jamaa amechemka kwani hakukuwa na umuhimu wa kutoa wimbo unaofanana na ule wa mwanzo na vilevile kushirikisha wasanii wenye majina kama Juma Nature na Mchizi Mox, Michano ya Mkola Man tuonane wiki ijayo