Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
Nahodha wa zamani wa Simba SC, Hassan Isihaka amekamilisha dili ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao.
Ndanda moja kati ya timu zinaxoshiriki Ligi kuu ya Tanzania bara imemsajili beki huyo wa kati aliyemaliza mkataba wake na kulikuwa na mpango wa kujiunga na Mbao FC ya Mwanza.
Isihaka ameshindwana na Simba baada ya kuitumikia kwa misimu miwili, msimu uliopita beki huyo aliyefanikiwa kubeba kombe la Mapinduzi na Ujirani mwema, alikorofishana na kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja raia wa Uganda