Na Salum Fikiri Jr DAR ES SALAAM
SIMBA SC imeanza harakati zake za kuimarisha kikosi chake baada ya kumleta beki kisiki anayedaiwa kuwa ni kiboko ya mshambuliaji hatari wa Yanga Donald Ngoma, Method Mwanjali raia wa Zimbabwe.
Licha kwamba beki huyo kudaiwa ni mzee ana miaka 33 lakini ana uwezo mkubwa wa kusakata kandanda Method ni chaguo la kiungo mwingine wa Simba anayedaiwa kutimkia Austria Justice Majabvi.
Endapo beki huyo ambaye pia anacheza kama kiungo mkabaji, atachukua nafasi ya Paul Kiongera, Tayari Simba imeshafanikiwa kuwasajili wachezaji watano wa ndani na sasa imegeukia wa kigeni