Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI anayeongoza kwa mabao Bruce Kangwa wa timu ya Ligi kuu nchini Zimbabwe ya Highlanders, amewasili nchinj leo tayari kabisa kujiunga na Azam FC inayonolewa na makocha raia wa Hispania.
Kangwa ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zimbabwe na anatoka kwenye klabu kongwe na kubwa nchini humo ametua leo akiwa tayari kurithi nafasi ya nahodha John Rafael Bocco ambaye ameshaonyeshwa mlango wa kutokea.
Mshambuliaji huyo aliyetupia magoli 20 kwenye ligi ya nchi hiyo inasemekana ni mkali kuliko mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma ambaye naye ni raia wa Zimbabwe