MAMBO UWANJANI YAMPA TUZO YA UCHEZAJI BORA KAMUSOKO WA YANGA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

JARIDA la michezo la Mambo Uwanjani limempa tuzo ya uchezaji bora kiungo wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC Thabani Michael Scara Kamusoko hasa baada ya kuzikonga mioyo ya watu.

Mhariri wa jarida hilo Exipedito Mataruma amesema Kamusoko ni mchezaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kufanya vizuri kwa kipindi chote alichojiunga na timu hiyo.

Kamusoko alijiunga na Yanga wakati wa usajili wa Dirisha dogo mwaka jana, alitua Jangwani akitokea timu ya FC Platinum ya Zimbabwe na ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwabwaga Juma Abdul pia wa Yanga na Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar