CHIDIABELE ARUDI STAND UNITED

Na Paskal Beatus, SHINYANGA

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union ya Tanga  Chidiabele Abaslimu amerejea kwenye timu yake ya zamani ya Stand United kwa mkataba wa miaka .miwili imefahamika.

Chidiabele alikuwa na wakati mzuri alipokuwa Stand mwaka juzi lakini alipojiunga na Coastal Union makali yake yakapotea ghafla na kuiacha timu hiyo ikishuka daraja.

Mshambuliaji raia wa Nigeria, alifunga mabao 10 wakati Saimon Msuva wa Yanga akiibuka mfungaji bora katika Ligi ya msimu wa 2014/15 ambapo Yanga SC ikatwaa ubingwa.

Lakini msimu uliopita, Chidiabere hakuwa katika msimu mzuri na kujikuta akipotezwa na wenzake, mshambuliaji huyo alifunga bao moja licha ya kucheza mechi kadhaa