Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
USIKU wa Julai 17, 2016 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndiyo Wadhamini wakuu wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara, walitangaza na kutoa tuzo 13 kwa wachezaji, refa na timu bora zilizofanya vizuri msimu wa 2015/16, Vodacom kwa kushirikiana na TFF wamefanikiwa kuchagua na kutoa zawadi kwa washindi wa tuzi hizo.
LISTI YA WASHINDI WA TUZI NA ZAWADI MBALIMBALI
Mchezaji bora wa Ligi kuu 2015/16 Juma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820.
Mfungaji bora ni Amissi Tambwe wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940.
Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein "Tshabalala" wa Simba Tsh Milioni 4.
Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940.
Kocha bora ni Hans Van der Pluijm wa Yanga Tsh Milioni 8.
Timu yenye nidhamu bora ni Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820.
Bingwa wa Ligi kuu ni Yanga Tsh Milioni 81,345,723.
Mshindi wa pili ni Azam FC Tsh Milioni 40,672,861.
Mshindi wa tatu ni Simba SC Tsh Milioni 29,052,044.
Mshindi wa nne ni Prisons Tsh Milioni 23,242,635.
Mfungaji bora wa goli zuri ni Ibrahim Ajibu wa Simba Tsh Milioni 3.
Refa bora ni Ngole Mwangole Tsh Milioni 5,742,940.
Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Scara Kamusoko wa Yanga Tsh Milioni 5