Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2018

KESSY AIPA POINTI TATU MUHIMU YANGA DHIDI YA NDANDA

Picha
Na Ikram Khamees. Mtwara Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imezidi kumfukuzia mtani wake wa jadi Simba kileleni, baada ya kuilaza Ndanda Fc mabao 2-1, mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Kwa ushindi huo sasa Yanga inafikisha pointi 40 ikiwa imeshuka dimbani mara 19 sawa na mahasimu wao Simba ambao wao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 45, Yanga walianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya 6 likifungwa na Pius Buswita akipokea pasi ya Hassan Kessy. Kabla ya mapumziko Hassan Kessy ambaye leo tena amekuwa lulu, aliifungia Yanga bao la pili na la ushindi, dakika ya 36  hata hivyo Yanga itajilaumu yenyewe kwa kukosa penalti iliyopigwa na Papy Kabamba Tshishimbi. Kipindi cha pili Ndanda nao walijipatia bao la kufuta machozi lililofungwa na Nassoro Kapama dakika ya 46 aliyepokea pasi ya Mrisho Ngasa "Anko", Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswa

JERRY MURO: CHIRWA SI WA KUMLINGANISHA NA OKWI KWA SASA, OKWI MTU MWINGINE BWANA!

Picha
Na Mwandishi Wetu Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameeleza mtazamo wake wa kuwa nani anaweza kuwa mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara. Muro amesema anampa nafasi kubwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kutokana na kiwango kizuri ambacho amekuwa akikionesha akiwa na Simba. Mbali na hilo, Muro pia amemtaja mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa kuwa hawezi kumfikia Okwi, kwani kiwango chake si kama cha mwenzake. Muro amesema Chirwa amekuwa akigoma kila wakati kuichezea hata timu yake, hivyo hampi na nafasi ya kuchuana na Okwi na akaenda mbali kwa kusema hastahili kulinganishwa naye. "Kwangu mimi Okwi ndiye mchezaji bora kwa sasa, hauwezi ukamlinganisha na Chirwa ambaye amekuwa akigoma hata kuichezea Yanga, Okwi ni ''Real Proffesional" hivyo hawezi kufikiwa na Chirwa katika mbio za ufungaji bora" alisema Muro. Okwi mpaka sasa amefikisha mabao 16 katika mechi 19 alizocheza msimu huu, wakati Chirwa ana mabao 11.  Emmanuel O

BODI YA LIGI YANYOOSHA MIKONO KWA YANGA

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Hatimaye Bodi ya Ligi (TPLB) imeridhia klabu ya Yanga iendelee na maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuisogeza mbele mechi yake dhidi ya Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Jumamosi ijayo ya Machi 3 uwanja wa Jamhuri Morogoro wa Ligi Kuu Bara huku ikishuka tena uwanjani Machi 6 kucheza na Township Rollers ya Botswana. Yanga iliiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wake angalau mmoja ili kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu michuano ya kimataifa, mabingwa hao kupitia katibu wao mkuu, Charles Boniface Mkwasa walikuwa wakilalamikia ufinyu wa ratiba yao. Yanga ilipangiwa mechi zake mfululizo, Jumapili ilucheza na Majimaji ya Songea mchezo uliofanyika Songea wa hatua ya 16 Bora kombe la Azam Sports Federation Cup, lakini pia ikapangiwa kucheza na Ndanda Jumatano kabla tena Jumamosi kupangwa kucheza na Mtibwa Sugar. Lakini Bodi ya Ligi imeamua kusogeza mbele mchezo wao wa VPL dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ilikuwa uchezwe Juma

SIMBA KANYAGA TWENDE HADI UBINGWA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, jioni ya leo wameendeleza ubabe wao baada ya kuichapa bila huruma Mbao Fc ya Mwanza mabao 5-0 uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Mbao Fc walionekana kuibana Simba dakika 20 za mwanzo wa mchezo lakini kocha wa Simba aliona udhaifu wa Simba na kuamua kumwingiza kiungo Mzamiru Yassin ambaye akaubadili mchezo na Simba kuanza kujipatia mabao mawili hadi mapumziko. Shiza Kichuya alianza kufunga dakika ya 38 kabla ya Emmanuel Okwi ajaongeza la pili dakika ya 41, kipindi cha pili Okwi tena akafunga la tatu dakika ya 68 wakati Erasto Nyoni akafunga la nne na Mghana, Nicolaus Gyan alihitimisha kalamu ya magoli kwa kufunga dakika ya 86. Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha pointi 45 wakiendelea kuongoza na sasa ikitanua gepu kubwa na mahasimu wao Yanga ambao wanafuatia kwa kushika nafasi ya pili, Yanga ina pointi 37 ikiachwa nyuma kwa pointi 7 Simba imeifunga Mbao mabao 5-0

SUGU AHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KUMTUSI RAIS MAGUFULI

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Mbunge wa Mbeya mjini na mwanamuziki maarufu wa Hip Hop hapa nchini, Joseph Osmund Mbilinyi, amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kumtukana Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Joseph Pombe Magufuli. Hakimu mkazi wa mahakama ya Mbeya mjini, Michael Mteite ametoa hukumu hiyo leo baada ya kujiridhisha kuwa Sugu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbeya kumtusi Rais wa nchi jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Mteite ametoa hukumu hiyo ili wabunge na watu wengine wasifanye hivyo kwani ni kosa kubwa kutoa lugha chafu kwa mtu mwingine pia kwa Rais wa nchi, licha ya Sugu kuhukumiwa miezi mitano, mahakama hiyo imemuhumu katibu wa chama hicho mkoani Mbeya, Emmanuel Masonga miezi sita naye akihusika kumtusi Rais Magufuli Joseph Mbilinyi amehukumiwa jela miezi kwa kumtukana Rais Magufuli

Kispoti

Picha
Yanga wapo katika wakati mgumu lakini........ Na Prince Hoza TANGU alipojiondoa Yusuf Mehbood Manji ambaye alikuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga morali imeshuka, fedha imetoweka hata kasi ya timu inaonekana kupungua. Uwepo wa Manji ndani ya Yanga uliwapa faida kubwa Wanayanga, Yanga imetawala soka la Tanzania takribani miaka mitano, huku ikiwateza mahasimu wao Simba Sc ambao ilifikia wakati ilipachikwa jina la utani la "Wamchangani" jina ambalo walibatizwa na aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro. Jerry Muro akaendelea kuibatiza majina mengine ya utani Simba na kuwakera mashabiki wake, Simba iliitwa "Wamatopeni" na hiyo yote ni kutokana na matokeo mabovu iliyopata. Uwepo wa Manji uliwafanya wachezaji wa Yanga waishi kifalme, Yanga iliweza kusajili wachezaji bora kutoka kila mahari, na ndio maana ikaweza kujiwekea historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara tatu mfululizo. Manji akaipoteza kabisa Simba ambayo ilishindwa kufu

Matokeo yoote kombe la Azam Sports Federation Cup

Picha
Mzunguko wa 4 wa michuano ya Azam Sports Federation Cup unaelekea kukamilika kesho Februali 25, 2018 na timu nane zitasalia kucheza robo fainali. Angalia matokeo yote na ratiba iliyobaki ya mechi mbili zitakazopigwa, Mwandishi wetu, Salum Fikiri Jr anatupasha. Njombe Mji 1 Mbao Fc1 (Penalti 6-5), Singida United 2 Polisi Tanzania 0, Azam Fc 3 KMC 1, Yanga 2 Majimaji 1, Mtibwa Sugar 3 Buseresere 0, JKT Tanzania 1 Ndanda Fc 0, leo ni Stand United va Dodoma Fc, CCM Kambarage na Kiluvya United vs Tanzania Prisons, Filbert Bayi Stadium, Kibaha Azam Fc imekata tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo

YANGA YATINGA ROBO FAINALI FA CUP

Picha
Na Mwandishi Wetu. Songea Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 2-1 uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma. Yanga walijipatia bao la kuongoza lililofungwa na kiungo mshambuliaji Pius Buswita kunako dakika ya 40, hadi mapumziko walikuwa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Majimaji nao walicharuka wakitaka kusawazisha. Lakini ukuta wa Yanga ulikuwa imara, dakika ya 57 Yanga walipata bao la pili lililofungwa na Emmanuel Martin aliyepokea pasi ya Hassan Kessy, vijana wa Majimaji walijipatia bao la kufutia machozi likifungwa na Jaffari Mohamed. Nayo Mtibwa Sugar imeungana na Yanga kucheza robo fainali baada ya kuilaza Buseresere ya Geita mabao 3-0 uwanja wa Nyamagana, Mwanza, michuano hiyo itaendelea tena kesho Kiluvya United ikiwakaribisha Prisons uwanja wa Filbert Bayi mjini Kibaha, na Stand United ikiwaalika Dodoma Fc Yanga Sc imeingia robo fainali ko

Singida United yaipigisha kwata Polisi Tanzania, lakini yapata pigo

Picha
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam Timu ya Singida United imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuipigisha kwata timu ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Namfua mjini Shinyanga. Ushindi huo wa leo moja kwa moja unawafanya waungane na Njombe Mji ya Njombe ambayo nayo iliwaondosha mashindanoni Mbao Fc kwa mikwaju ya penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Katika mchezo wa leo hadi mapumziko timu hizo mbili zilikuwa bila bila, Singida United walijipatia mabao yao kipindi cha pili kupitia kwa beki wake Kennedy Wilson dakika ya 70 na Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu dakika ya 77. Wakati huo huo uongozi wa Singida United unatoa salamu za pole kwa mchezaji wake Nizar Khalfan kwa kufiwa na mama yake mzazi Singida United imeifunga Polisi Tanzania leo

Wachezaji Majimaji wagoma kucheza na Yanga kesho

Picha
Nawandishi Wetu. Dar es Salaam Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu ya Majimaji Fc ya Songea wamegoma kuichezea timu hiyo hadi kuhatarisha uwepo wao kesho wakati timu yao itakapoumana na Yanga Sc mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup hatua ya 16 bora katika uwanja wa Majimaji. Kocha wa Majimaji Habibu Kondo ameingia mchecheto jana mazoezini baada ya wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza kugomea mazoezi wakishinikiza kulipwa fedha zao za usajili na mishahara. Kondo ilibidi awajumuhishe wachezaji wa kikosi cha pili wapatao 14 ili kesho Jumapili waweze kuivaa Yanga ambayo tayari imeshawasili Songea leo na ndege, lakini mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Ngonyani amesema kwa sasa suala lao wamelipeleka kwa mbunge wao Damas Ndumbaro na mambo yatakuwa safi Majimaji Fc wamegoma kucheza na Yanga kesho

Yanga yaifuata Majimaji kwa mwewe, yaapa kutinga robo fainali

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc wanatarajia kusafiri asubuhi ya leo kuelekea mjini Songea mkoani Ruvuma ambapo kesho Jumapili watashuka uwanja wa Majimaji kucheza na wenyeji wao Majimaji Fc hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup, maarufu FA Cup. Msafara wa nyota wa Yanga utaingia kwa ndege mjini Songea baadaye leo ukitokea jijini Dar es Salaam ambapo pia uliwasiri mapema juzi ukitokea Victoria nchini Shelisheli ulikoenda kucheza na Saint Louis Ligi ya mabingwa barani Afrika. Yanga ilifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na kutoka sare ya 1-1 ugenini, endapo Yanga ikifanikiwa kuifunga Majimaji itakuwa imeingia robo fainali, na kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa Yanga, Hussein Nyika, amesema wataendeleza ubabe kwa Majimaji kesho. Yanga iliifunga Majimaji mabao 4-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Sa

LEO NI VITA KALI YA POLISI TANZANIA NA WAKULIMA WA ALIZETI, NAMFUA

Picha
Na Ikram Dar es Salaam Michuano ya Azam Sports Federation Cup leo inaendelea tena kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti hapa nchini, lakini vita kali itapigwa jioni kule kwenye dimba la Namfua mjini Singida likiwahusisha wenyeji Singida United na Polisi Tanzania. Hiyo itakuwa moja kati ya mechi kali na ngumu kutokana na ushindani wenyewe wa michuano hiyo iliyofikia hatua ya 16 bora, tayari timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe imeshatangulia robo fainali baada ya kuiondosha Mbao Fc ya Mwanza kwa mikwaju ya penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Lakini pia usiku wa leo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kutapigwa mchezo mwingine mkali kati ya vijana wa Manispaa ya Kinondoni, KMC wanaonolewa na beki na kocha wa zamani wa Yanga, Fred Minziro, watakapoumana na Azam Fc. Michuano hiyo itaendelea tena kesho Jumapili ambapo Majimaji ya Songea itawaalika Yanga katika uwanja wa Majimaji, na Buseresere itawakaribisha Mtibwa Sugar, Jumatatu, Kiluvya United itaikari

SIMBA WASEMA HAWAIOGOPI AL MASRY

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Uongozi, wanachama na wapenzi wa wawawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Simba Sc wamesema hawaiogopi wala kuihofia hata kidogo timu ya Al Masry ya Misri ambao ni wapinzani wao katika mchezo ujao. Akizungumza na mtandao huu, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema klabu yake haina hofu kabisa na mchezo huo kwani wao hesabu zao ni kusonga mbele. Manara ameyasema hayo juzi mara baada ya Simba kufanikiwa kuingia raundi ya pili ya kombe la Shirikisho kwa kuitoa mashindanoni timu ya Gendarmarie ya Djibout kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya ushindi wa 4-0 nyumbani na 1-0 ugenini. Simba hawaihofii Al Masry hata kama inatokea Misri ambapo timu zake zimekuwa zikizisumbua timu za Tanzania, lakini Manara akakumbushia pale Simba ilipoitoa nishai Zamalek mwaka 2003 ambapo amedai wembe uleule walioutumia kwa Zamalek watautumia kwa Al Masry Simba wamesema hawaiogopi Al Masry hata kidogo

STAA WETU

Picha
NI JUMA MAHADHI, KIUNGO MSHAMBULIAJI ANAYEPANDA KIWANGO NA KUSHUKA. Na Prince Hoza WASWAHILI husema maisha ni kupanda na kushuka, kuna wakati maisha yanakuwa fresh, na kuna wakati maisha yanabadilika na kuwa hovyo kabisa kiasi kwamba unaomba ardhi ipasuke. Lakini hayo ndiyo maisha aliyopangiwa mwanadamu, wanasema mwanadamu furaha kwake huwa ni kidogo sana lakini shida hutawala, watu wengi wanapitia msoto huo, mmoja wapo ni kiungo mshambuliaji wa Yanga Sc, Juma Mahadhi. Kuna wakati Mahadhi alikuwa katika kipindi kizuri sana kiasi kwamba wengi tuliamini kwamba atakuja kuwa tegemeo kwenye kikosi cha Yanga, Mahadhi alizaliwa jijini Tanga miaka 23 iliyopita na anatokea kwenye ukoo wa wanasoka. Mahadhi ni mjukuu wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Omary Mahadhi Bin Jabir ambaye pia amewahi kuzichezea kwa mafanikio African Sports "Wanakimanumanu" ya Tanga na Simba Sc ya jijini Dar es Salaam. Enzi zake Omary Mahadhi alisifika kwa kudaka kama nyani na ndiye aliyeiwezesha

RAIS WA FIFA AAHIDI NEEMA TANZANIA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani, (FIFA)  Gianny Infatinho amemuahidi Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa kuwa Shirikisho lake litawekeza nchini. Bosi huyo wa Fifa ameyasema hayo leo Magogoni Dar es Salaam alipomtembelea waziri mkuu, Infantinho amedai Tanzania ni sehemu nzuri kuwekeza kutokana na amani na utulivu uliopo. Uongozi wote wa Shirikisho la soka ulimwenguni pamoja na wa mabara yote waliwasili jana nchini kuanza mkutano mkubwa wa Shirikisho hilo ambapo Tanzania inawakilishwa na Rais wa Tff, Wallace Karia, Kaimu katibu mkuu, Wilfred Kidao na mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga Rais wa Fifa Gianny Infatinho (Kushoto) akiwa na waziri mkuu, Kassim Majaliwa leo

MASIKINI HIMID MAO, KUKAA NJE WIKI SITA

Picha
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam Kiungo wa mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc Himid Mao Mkami atalazimika kukaa nje kwa kipindi cha wiki sita kuuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini, kiungo huyo alianza kukosekana katika michezo kadhaa ya timu yake ya Azam Fc na kupelekea kuyumba kwa kikosi hicho. Mao ambaye anafahamika kwa jina la Ninja kutokana na uchezaji wake, aliumia akiwa na kikosi hicho na alishindwa kuendelea kuichezea timu hiyo ambayo imempa majukumu ya unahodha. Azam Fc mpaka sasa inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 huku ikishuka uwanjani mara 19, kikosi hicho kitaumana na KMC siku ya Jumamosi katika michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya 16 Bora Himid Mao atakaa nje kwa muda wa wiki sita

Township Rollers yaifuata Yanga Ligi ya mabingwa Afrika

Picha
Hatimaye sasa klabu bingwa ya Tanzania Bara, Yanga Sc itaumana na timu ya Township Rollers ya Botswana katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika. Yanga jana imevuka raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Saint Louis ya Shelisheli ambapo jana walitoka nayo sare ya 1-1 katika uwanja wa Linite mjini Victoria. Lakini wawakilishi wa Botswana, Township Rollers wao walifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza baada ya kupita kwa jumla ya mabao 4-2 hasa baada ya jana kufungwa na wenyeji El Marreikh ya Sudan mabao 2-1, mchezo wa kwanza Township Rollers ilishinda mabao 3-0 nyumbani Wachezaji wa Township Rollers ya Botswana wakishangilia

Yanga yatinga raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Afrika

Picha
Na Paskal Beatus. Victoria Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuingia raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare na wenyeji Saint Louis ya Shelisheli ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Linite mjini Victoria. Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na Yanga wakafanikiwa kujipatia bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ajibu aliyepokea pasi ya Hassan Kessy dakika ya 45. Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele, kipindi cha pili wenyeji Saint Louis walijaribu kulifikia lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Betrand Esther Ibrahim Ajibu (Wa kwanza kulia) akishangilia moja ya magoli aliyofunga

Niyonzima aenda India kutibiwa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo wa kimataifa wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, amesafiri leo kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu yake ya goti linalomsumbua. Niyonzima aliyehamia Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mahasimu wao Yanga Sc, aliweza kuitumikia Simba mwanzoni mwa msimu na kuumia goti lililomtesa kipindi chote mpaka leo kupaa zake kwenda India. Uongozi wa Simba umehakikisha mchezaji huyo muhimu anatibiwa upesi ili kuungana na wenzake, Said Mohamed Nduda naye alienda kutibiwa India na sasa amerejea uwanjani Haruna Niyonzima ameondoka leo kuelekea India kutibiwa

Simba yaendeleza ubabe kwa Gendarmarie

Picha
Na Mwandishi Wetu. Djibout Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba Sc jioni ya leo imeendeleza ubabe baada ya kuichapa bao 1-0 mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho barani Afrika. Simba imepata ushindi huo ugenini leo na kufanikiwq kuingia Raundi ya kwanza kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-0, kwa ushindi huo sasa Simba itaumana na El Masry ya Misri ambayo nayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 4-0 dhidi ya Green Buffoeroes ya Zambia. Goli lililoipa ushindi Simba leo lilifungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa, Mganda Emmanuel Okwi Simba Sc imeifunga Gendarmarie leo

Kispoti

Picha
NAUONA MWISHO MBAYA WA TSHABALALA SIMBA. Na Prince Hoza HALI si shwari kwa maisha ya Mohamed Hussein "Tshabalala" au Zimbwe Jr ndani ya klabu ya Simba, na hii yote inatokana na usajili uliofanywa na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu. Simba imefanya usajili mkubwa wa kuongeza wachezaji wapya 13 ambao wameweza kuleta chachu kwenye kikosi hicho ambacho kwa sasa kinaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 ikishuka dimbani mara 18 ikifuatiwa na mahasimu wao Yanga Sc wenye pointi 37 nao wamecheza mechi 18. Azam Fc inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 yenyewe ikicheza mechi 19, Singida United inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 34 nayo ikicheza mechi 19. Katika misimu miwili iliyopita, Mohamed Hussein "Tshabalala" alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, Tshabalala pia ameweza kushinda tuzo mbalimbali za uchezaji bora za klabu na za Ligi Kuu ya Vodacom. Lakini kubwa zaidi ni pale alipoweza kuzoa tuzo mbili

AZAM YAJIONDOA MBIO ZA UBINGWA, YABANWA NA LIPULI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Iringa Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imelazimishwa sare tasa 0-0 na wenyeji Lipuli Fc mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Samora mjini Iringa. Matokeo hayo yanazidi kuwaondoa Azam kwenye mbio ya ubingwa na kuzipisha Simba na Yanga zikichuana kileleni huku pia ikiwapa nafasi Singida United kuwakimbiza. Azam Fc imefikisha pointi 35 katika michezo 19 waliyocheza, Lipuli nao wanafikisha pointi 20 pia wakicheza mechi 19. Azam Fc imeanza kujiondoa kwenye ubingwa

STAA WETU

Picha
: NI ASANTE KWASI, ANAYETEMBEA NA UBINGWA WA SIMBA. Na Prince Hoza Simba Sc ina muunganiko mzuri kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo hadi ushambuliaji, na hiyo ndiyo imeifanya klabu hiyo iliyozaliwa mwaka 1936 kuongoza ligi kwa tofauti kubwa ya pointi baina yake na wanaomfuatilia. Kasi ya Simba imezidi kuongezeka katika mzunguko wa pili, Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 42 ikicheza mechi zake 18 pamoja na ule wa jana dhidi ya Mwadui Fc ulioisha kwa sare ya 2-2 uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Vinara hao wamewaacha mbali wapinzani wake Yanga, Azam na Singida United ambao wanawafuatilia kwa nyuma, kikosi hicho kinachonolewa na Mfaransa, Pierre Lechantre na msaidizi wake Masoud Djuma raia wa Burundi kimeonekana kuwa imara msimu huu na kinaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Chachu ya ushindi iliyopo katika klabu ya Simba haiji bure isipokuwa inatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kwa wachezaji wa kikosi hicho, miongoni mwa wachezaji tegemeo ni Asante Kw

Hatimaye ndoa ya Diamond na Zari yavunjika rasmi

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Zarinah Hassan(Zari) ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva nchini humo, Nasibu Abdul(Diamond Platnumz) Kwa kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii wa Instagaram, Zari amesema kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano Zari na Diamond katika kipindi chao cha mahusiano kilichodaiwa kuanza Novemba 2014 wameweza kupata watoto wawili, Tiffah na Nillan Diamond na mkewe Zari kabla haeajaachana

Mwadui Fc kuishika sharubu Simba leo

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Timu ya Mwadui Fc ya mkoani Shinyanga, jioni ya leo inatelemka uwanja wa CCM Kambarage kuwakaribisha Simba Sc ya Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mwadui inayomakata nafasi ya 12 ikiwa na pointi 18 itaingia uwanjani kwa lengo la kuishika sharubu Simba hasa ikitaka ushindi ili kuchupa hadi nafasi ya 7, pia wanahitaji kushinda ili kulipiza kisasi baada ya kufungwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam. Kikosi hicho kitaingia uwanjani kikijivunia nyota wake Awesu Awesu, Awadh Juma na Hassan Kabunda kwa vyovyote kinaweza kuibuka na pointi tatu muhimu, lakini Simba nao wanataka kujiimarisha kileleni kwani hadi sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 41 ikifuatiwa kwa karibu na hasimu wake Yanga mwenye pointi 37. Simba itaingia uwanjani ikitaka kuendeleza wimbi la ushindi ili ijiwekee mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Bara, Simba itawategemea zaidi nyota wake Emmanuel Okwi raia wa Uganda, Shiza Kichuya na

Tshishimbi aing' arisha Yanga, ikiipiga 4G Majimaji

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imeendelea kutakata baada ya kuichapa Majimaji ya Songea mabao 4-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ushindi huo moja kwa moja unaifanya Yanga ifikishe pointi 37 sasa ikiwa nyuma ya pointi nne na mahasimu wao Simba Sc wanaokamata usukani wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 41 lakini wana mechi moja mkononi. Furaha ya Wanayanga ilianzia dakika ya 18 ilipoandika bao la kwanza lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na kiungo wake Mkongoman, Papy Kabamba Tahishimbi kabla ya Mzambia Obrey Chirwa kufunga bao la pili dakika ya 29. Yanga waliongeza bao la tatu dakika ya 43 lililofungwa kwa shuti kali na winga, Emmanuel Martin, hadi mapumziko Wanajangwani hao walikuwa mbele kwa mabao hayo, kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini Majimaji waliokuwa pungufu baada ya beki wake Mwakanjuki kutolewa kwa kadi nyekundu nao walipata penalti dakika ya 56 iliyowapa bao la kwanza lilil

CHIRWA KUSAKA HAT TRICK NYINGINE LEO

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Uhuru zamani ukijulikana Taifa. Mabingwa watetezi Yanga Sc watashuka dimbani kuumana na Wandengeleko Majimaji Fc toka Songea mechi ikipigwa jioni ya leo. Kocha mkuu wa Majimaji, Habib Kondo yeye amejinasibu kupata matokeo katika mchezo huo huku msemaji wa Yanga, Dissmas Ten ametamba kushinda mchezo huo ili waweze kutetea ubingwa wao wa Bara. Lakini mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, anatarajia kuongeza idadi ya mabao ili aweze kutwaa kiatu cha dhahabu, Chirwa ana mabao 10 akiwa nyuma ya Mganda, Emmanuel Okwi mwenye mabao 13. Chirwa alifunga mabao matatu peke yake katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji ambapo Yanga ilishinda mabao 4-0, hivyo na leo tena Chirwa anatarajia kupiga hat trick nyingine Obrey Chirwa anasaka hat trick nyingine leo

SIMBA WATUA SALAMA SHINYANGA, KUWAVAA MWADUI KESHO

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Kikosi cha wachezaji wa Simba Sc wametua salama leo mjini Shinyanga baada ya safari yao waliyoianza alfajili ya leo kwa kutumia usafiri wa ndege. Simba Sc inayoongoza Ligi Kuu Bara imetua salama na kesho jioni itakuwa mgeni wa timu ya Mwadui Fc katika uwanja wa Mwadui Complex, katika mchezo wa kwanza Simba iliifunga Mwadui mabao 3-0. Ligi hiyoinaendelea leo kwa mchezo mmoja tu ambapo bingwa mtetezi Yanga Sc itakapowaalika Majimaji Songea katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam Simba Sc wamewasili salama mjini Shinyanga kesho wanacheza na Mwadui

ALIYEVUMA

Picha
RAMADHAN LENNY, KIUNGO BORA ALIYEPITA MSIMBAZI. Na Shafih Matuwa Jina la Ramadhan Lenny Maufi si geni masikioni mwa wapenzi wa mpira wa miguu hapa nchini hasa wale wa miaka ya 90, kwa vijana wa kileo inawezekana ikawa changamoto kumfahamu. Na ndio maana Mambo Uwanjani imeamua kuwaletea makala fupi ya kuwakumbusha nyota waliopata kutamba huko nyuma tena wale WALIOVUMA. Leo hii tumemmulika kiungo fundi kabisa ambaye inasemekana hajawahi kutokea katika kikosi cha Simba kwa misimu yote tangia ilipoanzishwa mwaka 1936, si mwingine ni Ramadhan Lenny Maufi ambaye kwa sasa ni marehemu. Lenny alikuwa kiungo mkabaji namba sita ambaye hakuna mfano wake tena, hata hao akina Seleman Matola, Jonas Mkude na wengineo hawamfikii. Lenny amekufa na ubora wake, aliisaidia Simba kutamba katika ngazi mbalimbali za ndani na nje, Simba kuchukua ubingwa wa Bara haikuwa shida kama ilivyo sasa inasotea mwaka wa tano huu haijachukua. Simba ilikuwa ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya muungano wakati huo ilikuwa

RAIS MAGUFULI KUMLAKI RAIS WA FIFA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli anatazamiwa kuupokea ugeni mzito wa Shirikisho la kandanda duniani, (FIFA) unaotarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo. Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni, Mhe Harrison Mwakyembe inasema kuwa Rais Magufuli ataupokea ugeni huo na kufanya mazungumzo na Rais wa Fifa, Gianni Infantinho. Mwakyembe leo alikuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambapo amedai serikali imeamua kuisaidia TFF katika mapokezi ya viongozi hao wa soka duniani. Infantinho atapokewa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF) Ahmad Ahmad, mkutano mkuu wa Fifa utafanyika hapa nchini na kwa mujibu wa Mwakyembe, amedai hata kama Rais Magufuli atashindwa kuhudhuria basi atawakilishwa na makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan au waziri mkuu, Kassim Majaliwa Rais John Magufuli atampokea Rais wa Fifa wiki ijayo

NYOSO AFUNGIWA MECHI 5 KWA KUMDUNDA SHABIKI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Beki wa Kagera Sugar "Wana mkurukumbi", Juma Said Nyoso amefungiwa mechi tano pamoja na kupigwa faini ya shilingi Milioni moja kwa kitendo cha kumpiga shabiki wa Simba Sc. Kamati ya masaa 72 ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) imetoa adhabu hiyo kwa beki huyo mtukutu aliyewahi pia kuzichezea Ashanti United, Simba Sc, Coastal Union na Mbeya City. Beki huyo alimpiga vibaya shabiki wa Simba Sc katika uwanja wa Kaitaba Bukoba wakati Simba ilipoumana na Kagera Sugar, kamati hiyo imemkuta Nyoso ana hatia ya kumpiga shabiki huyo aliyekuwa akishangilia ushindi wa timu yake ya Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar. Nyoso alimpiga mateke shabiki huyo anayedaiwa kumpulizia vuvuzela masikioni mwake, awali Nyoso aliwahi kufungiwa miaka miwili baada ya kumtomasa makalioni nahodha wa zamani wa Azam Fc, John Raphael Bocco Juma Nyoso amefungiwa mechi tano kwa kupiga shabiki

MKOLA MAN ASEMA DIAMOND NA JUX NI FREEMASON WALIOKOMAA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Tanga Mwanahip hop anayetamba na wimbo wake "Swali ndiyo jibu" , Christian Mhenga maarufu Mkola Man jana wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, 'Birthday' aliweka wazi majina ya wasanii wanaoamini Freemason hapa nchini. Mkola Man ambaye naye alikuwa mmoja ya waumini wa imani hiyo inayodaiwa ni ya kishetani inayomfanya muumini wake kupata mafanikio ya haraka, aliwataja wasanii maarufu nchini wanaoshabikia imani hiyo. Mambo Uwanjani ilikuwemo mjini Hale mkoani Tanga ambapo msanii huyo aliwaalika ndugu jamaa na marafiki zake ambapo aliweka wazi kuwa msanii Diamond Platinum ni nguzo ya freemason sambamba na Juma Jux na Young Killer. Mkola Man ambaye alilazimika kuhama kwao kisa kutumikia imani hiyo kabla ajawaangukia wazazi wake na kutubu, amedai wasanii hao wamekuwa watumwa wa imani hiyo kwa kuvaa vidani vinavyoaminika kuwa vya freemason Diamond Platinum inasemekana no freemason

Yanga vitani kesho na Majimaji

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc kesho Jumatano wataikaribisha Majimaji Fc mchezo wa Ligi Kuu Bara uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Yanga inayokamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 34 ikiachwa nyuma kwa pointi saba na mahasimu wao Simba Sc ambao wana pointi 41 wanatazamiwa kufanya vema zaidi ili kuikaribia Simba ambayo yenyewe itashuka uwanjani keshokutwa Alhamis. Simba itakuwa ugenini Shinyanga itakapowafuata Mwadui Fc katika uwanja wa Mwadui Complex, awali mechi hizo ilikuwa zichezwe mwishoni mwa wiki lakini kutokana na vilabu hivyo viwili kukabiliwa na mechi za kimataifa, Bodi ya Ligi ikaamua kuzirejesha nyuma mechi hizo hadi Jumatano na Alhamis Yanga kesho wanacheza na Majimaji

Kagera Sugar yaishika koo Azam

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Timu ya soka ya Kagera Sugar ya Misenyi mkoani Kagera jioni ya leo imeikaba koo Azam Fc na kwenda nayo sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kwa matokeo hayo Kagera Sugar imepanda kwa nafasi moja kutoka mkiani hadi ya 16 kwa kufikisha pointi 14 na mechi 18 huku Azam Fc ikibaki nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 34 sawa na Yanga tofauti yao ni magoli ya kufunga na kufungwa. Timu hizo hadi zinaenda kupumzika dakika 45 zilikuwa hazijafungana, kipindi cha pili Kagera Sugar walitangulia kupata bao la kuongoza lililofungwa na beki Eladslaus Mfulele dakika ya 50 kabla ya Azam Fc kusawazisha kupitia kwa Iddy Kipagwile dakika ya 53 Kagera Sugar wameishika koo Azam Fc leo

Selembe atimka Majimaji

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji Seleman Kassim Selembe inasemekana ametimka katika kikosi cha Majimaji Fc ya Songea na kuonekana visiwani Unguja. Afisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru amethibitisha kutimka kwa mchezaji huyo ambaye aling' ara katika michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya, Desemba mwaka jana. Kwa mujibu wa Ndunguru, Selembe bado ana mkataba ba Majimaji hivyo kitendo chake cha kutoroka ni utovu wa nidhamu, lakini awali Selembe aliufuata uongozi wa Majimaji na kuwataka wavunje naye mkataba ili akajiunge na DC Motema Pembw ya DR Congo iliyoonyesha nia ya kumsajili baada ya kuvutiwa naye kwenye Chalenji. Uongozi wa Majimaji umegoma kumwachilia mchezaji huyo aende bure Motema Pembe na imewataka Wakongoman hao wafanye nao mazungumzo ili wawauzie Selembe, inasemekana Motema Pembe hawako tayari kuvunja mkataba ila wanamtaka Selembe bure Seleman Kassim.Selembe ametimka Majimaji

Kispoti

Picha
Yanga na nyie jengeni utaratibu wa kuwatibia wachezaji wenu nje ya nchi. Na Prince Hoza YANGA SC juzi imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Saint Louis ya Shelisheli mchezo wa Raundi ya awali Ligi ya mabingwa barani Afrika katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa maana hiyo Yanga inahitaji kujilinda zaidi ugenini zitakaporudiana ili isiruhusu kipigo cha mabao 2-0 kwani ikipata kipigo hicho itakuwa imeondoshwa mashindanoni, tatizo kubwa kwa upande wa Yanga lilionekana kwenye sehemu ya ufungaji. Yanga ilishindwa kupenya ukuta wa Saint Louis, hadi mapumziko timu hizo zilienda zikiwa hazijafungana, Yanga iliongoza kwa kumiliki mpira ikishambulia mara kwa mara, mabeki wa Saint Louis walikuwa imara kuzuia hatari zote. Wachezaji karibu wote wa Saint Louis walirudi nyuma kuzuia wasifungwe mabao mengi, kwa upande wa Yanga tatizo lilionekana kwenye sehemu ya ushambuliaji kwani hawakuwa na mtu mwenye uwezo wa kuingia na mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Saint Louis. Obrey

Stand United yaizamisha Singida United

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga, jana imeifunga Singida United bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Namfua mkoani Singida. Huo ni mwendelezo mzuri kwa Stand United ambao wameanza kujiondoa taratibu katika janga la kushuka daraja lakini pia yamekuwa matokeo mabaya kwa Singida United inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm katika vita ya kuwania ubingwa wa bara. Endapo Singida United ingeibuka na ushindi katika mchezo huo ingepaa hadi nafasi ya pili kwakufikisha pointi 36, sasa inabaki katika nafasi yake ya nne ikiwa na pointi 33 wakati Stand iliyokuwa nafasi ya 12 na pointi zake 16 sasa inakwea hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 19 sawa na Mbao Fc ambao nao wametoka sare tasa 0-0 na Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Matokeo mengine, Njombe Mji Fc ililazimishwa sare tasa na Mbeya City uwanja wa Sabasaba Njombe, na kikosi cha Ruvu Shooting kikaikandika Lipuli Fc ya Iringa mabao 3-1 uwanja wa Mabatini, Mland

Simba yaitandika Gendarmarie 4-0 mbele ya mzee Ruksa

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba Sc jioni ya leo imeichakaza bila huruma timu ya Gendarmarie ya Djibout mabao 4-0 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ikicheza mbele ya mgeni wa heshima, Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ally Hassan Mwinyi, Simba ilianza kuwainua vitini mashabiki wake waliojitokeza kuishuhudia, goli likifungwa dakika ya kwanza na Said Ndemla. Furaha ya mabao iliendelea tena katika dakika ya 33, nahodha John Bocco "Adebayor" aliipatia bao la pili kabla tena dakika ya 45 kufunga la tatu. Hadi wanakwenda mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa mabao hayo matatu, kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini vijana wa Gendarmeria walionekana kujilinda zaidi ili wasifungwe magoli mengi. Emmanuel Okwi aliipatia Simba bao la nne dakika tatu za nyongeza, kwa ushindi huo Simba imejiweka katika mazingira mazuri ya kusonga Raundi ya kwanza na kuna uwezekano wa kukutana na El Ma

BOCCO AWA MWANASOKA BORA WA MWEZI JANUARI, VPL

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Nahodha na mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, John Raphael Bocco "Adebayor" ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Bocco ameshinda tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kuwashinda Emmanuel Okwi pia wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui Fc, mshambuliaji amefanya vizuri katika mwezi Januari na kuisaidia timu yake kushinda mechi tatu akishiriki kikamilifu kwa mechi zote. Kwa mujibu wa kamati ya tuzo kwa kushirikiana na makocha, wamejiridhisha kumpa Bocco tuzo hiyo hasa baada ya kuimarika kwa kiwango, hadi sasa Bocco amefunga jumla ya mabao tisa akishikilia nafasi ya tatu. Tuzo hiyo msimu huu ilianza kwenda kwa Mganda Emmanuel Okwi aliyeshinda Agosti, Septemba ilienda kwa Shafik Batambuze naye ni Mganda wakati Oktoba ilienda kwa Mzambia Obrey Chirwa. Wengine walioshinda tuzo hiyo ni Mudathir Yahya mwezi Novemba na Habibu Kiyombo aliyeshinda mwezi Desemba, Bocco sasa atajinya

MSUVA APIGA HAT TRICK, CHAMA LAKE LIKIIUA BENFICA 10-0

Picha
Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameendelea kutakata katika klabu yake mpya ya Difaa El Jadida ya Morocco baada ya usiku wa jana kuifungia mabao matatu katika ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau, mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika uwanja wa Ben Ahmed mjini Jadida, Mazghan, Morocco. Msuva aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga Sc ya Tanzania, aliweza kufunga mabao yake hayo katika dakika za 44, 72 na 88. Mabao mengine ya Difaa El Jadida yamefungwa na Bakary N' diaye aliyefunga matano  dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na lingine likafungwa na Bilal El Magri dakika ya 54 Simon Msuva aliyebebwa, amefunga magoli matatu timu yake ikishinda 10-0

LEO NI ZAMU YA WEKUNDU WA MSIMBAZI KIMATAIFA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc jioni ya leo inatupa kete yake ya kwanza kimataifa itakapowakaribisha timu ya Gendermarie Tnale ya Djibout mchezo wa Raundi ya awali kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Simba inarejea kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo baada ya kusota kwa miaka minne kutafuta nafasi ya kushiriki, na kipindi chote imekuwa ikihaha kubadili makocha ili angalau ijipatie tiketi hiyo na mwaka jana Mcameroon Joseph Omog akaiwezesha kutwaa kombe la FA na mwaka huu kurejea kimataifa. Ikiingia katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi mnono ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele zitakaporudiana juma lijalo, Simba leo itawategemea zaidi nyota wake kama Emmanuel Okwi, John Bocco "Adebayor", Shiza Kichuya, Erasto Nyoni, Asante Kwasi na mlinda mlango wake Aishi Manula. Wawakilishi wengine wa Tanzania Yanga Sc jana ilipata ushindi kiduchu kwa kuilaza Saint Louis ya Shelisheli bao 1-0 katika uw

MAHADHI AIBEBA YANGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kusonga mbele katika michuano ya kimataifa, baada ya kuilaza Saint Louis ya Shelisheli bao 1-0 mchezo wa Raundi ya awali, Ligi ya mabingwa barani Afrika, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo haukuwa rahisi kwa Yanga kama watu walivyodhani kwani ilisubiri hadi kipindi cha pili dakika ya 66 kupata bao la ushindi lililofungwa na kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi aliyeunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Geofrey Mwashiuya. Vijana wa Saint Louis waibana vilivyo Yanga na kulifikia mara kwa mara lango isipokuwa umahiri wa kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili kulisaidia kuokoa hatari zote. Yanga sasa itakuwa na kazi ugenini ya kuzuia isifungwe mabao 2-0 kwani ikikubali kichapo hicho itayaaga mashindano hayo, Obrey Chirwa alikosa penalti kipindi cha kwanza baada ya Hassan Kessy kufanyiwa faulo kwenye eneo la hatari Juma Mahadhi ameibeba Yanga leo

OKWI AFICHUA KILICHOMRUDISHA VPL

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Sc, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, hatimaye ameweka wazi kufeli kwake kucheza soka la kulipwa katika nchi za Tunisia na Denmark. Kinara huyo wa magoli, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) amefichua kuwa, alishindwa kucheza nchini Tunisia na kuvunja mkataba na klabu ya Etoile du Sahel aliyojiunga nayo akitokea Simba Sc ya Tanzania ni kwa sababu timu hiyo ilishindwa kumlipa mshahara wake wa miezi mitatu. Okwi amesema timu hiyo ilianguka kiuchumi na ikajikuta ikishindwa kuwalipa wachezaji wake wengi na wengine kutimka, pia akaelezea kushindwa kwake Denmark na kuvunja mkataba na klabu ya Sonderjyske baada ya timu hiyo kushindwa kumpa nafasi ya kucheza. "Sikuwa chaguo la kwanza kwenye klabu hiyo hivyo nikapoteza nafasi kwenye timu ya taifa ya Uganda na sikuweza kuitwa tena kwenye timu hiyo hivyo nikakaa chini na viongozi pamoja na wakala wangu na kuamua kuvunja mkataba ili nikatafute nafasi kwingine", alis

YANGA KUTUPA KARATA YAKE YA KWANZA KIMATAIFA LEO

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo wanaanza kampeni yao ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Afrika itakapowakaribisha mabingwa wa Shelisheli, Saint Louis mchezo wa Raundi ya awali, uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Wawakilishi hao wa Tanzania wataingia uwanjani wakiwa na matumaini tele hasa baada ya kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake waliokuwa nje wakiuguza majeraha yao. Kwa bahati nzuri kipa tegemeo Mcameroon, Youthe Rostand atarejea langoni baada ya kukosekana, Rostand aliumia katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc, mbali na Rostand, nyota wake wengine Ibrahim Ajibu, Juma Abdul, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Andrew Vincent waliungana na wenzao kujiandaa na mchezo huo wa leo. Mabingwa hao wa Bara wamekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi zao za ndani hivyo inawapa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo na itawategemea zaidi nyota wake Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita na Obrey Chirwa ambao wanaunda kombinesheni hatari

Tenga, Mwenyekiti mpya BMT

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mhe Harrison Mwakyembe amemteua Leodegar Chila Tenga kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT) akimrithi Dioniz Malinzi aliyefutwa kazi. Tenga amewahi kuhudumu kama Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) ataanza majukumu hayo kuanzia sasa na pia ana kazi kubwa kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars iliyobahatika kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za mataifa Afrika zilizofanyika Lagos Nigeria mwaka 1980, pia amewahi kuzichezea Yanga Sc na Pan Africans Leodegar Tenga mwenyekiti mpya wa BMT

Manara awaangukia Yanga

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara "Computer" ni kama amewaangukia Yanga, baada ya kuwataka wapenzi na mashabiki wa Simba kuacha kuizomea Yanga kesho, itakapocheza na timu ya Saint Louis ya Shelisheli. Yanga Sc kesho inacheza na Saint Louis ya Shelisheli katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Barani Afrika. Imekuwa kawaida mashabiki wa Simba au Yanga kushangilia timu za nje zinapokutana na Simba au Yanga, hivyo Manara anawaomba Simba wenzake kuishangilia Yanga kesho ili mashabiki wa Yanga nao wawashangilie Jumapili ya keshokutwa watakapoumana na Gendarmerie ya Djibout zitakapoumana uwanja wa Taifa Dar es Salaam raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika Haji Manara amewataka mashabiki wa Simba kushangilia Yanga kesho

Ruvu Shooting yaiweka "Danger Zone" Kagera Sugar

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, jana jioni imeichapa Kagera Sugar mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi Kibaha Pwani. Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting inayonolewa na Abdulmatik Haji kufikisha pointi 17 na kuchupa hadi nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku sasa ikiiweka shakani Kagera Sugar ikichungulia tundu la kushuka daraja. Mabao ya Ruvu Shooting yenye msemaji wake asiyeishiwa maneno, Masau Bwire yalifungwa na Khamis Mcha "Vialii" dakika ya 55 na Alinanuswe Martin dakika ya 79 Ruvu Shooting imeifunga Kagera Sugar

Staa Wetu

Picha
Habibu Kiyombo: anakuja ado ado. Na Prince Hoza HUWEZi Kuamini ninachokiandika, ila ukweli huko hivyo, Habibu Haji Kiyombo ndiyo mwanasoka wa kwanza Tanzania Bara msimu huu kutangazwa mchezaji Bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Ikumbukwe kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo ya mwanasoka Bora wa mwezi wa VPL alikuwa Mzanzibar, Mudathir Yahya Khamis, Kiyombo amekuwa Mtanzania Bara wa kwanza kushinda tuzo hiyo. Emmanuel Okwi raia wa Uganda anayekipiga Simba Sc  alishinda tuzo hiyo mwezi Agosti, wakati Shafik Batambuze naye raia wa Uganda, anayekipiga Singida United akashinda Septemba. Baada ya hapo tuzo ikaenda kwa Mzambia, Obrey Chirwa wa Yanga Sc aliyeshinda Oktoba kisha ikaenda kwa Mzanzibar, Mudathir Yahaya wa Singida United mwezi Novemba kabla ya Desemba tuzo kwenda kwa Habibu Kiyombo ambaye ni mshambuliaji wa timu ua Mbao Fc ya jijini Mwanza. Haikuwa rahisi Kiyombo kushinda tuzo hiyo kwani aliweza kuwabwaga John Raphale Bocco "Adebayor"